Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Kijiji Cha Nyuki co ltd, Tanzania Apr. Philemon Josephat Kiemi amesema Kampuni anayoiongoza ipo kwenye hatua za Mwisho za kukamilisha Ujenzi wa Chuo kikuu Cha Nyuki Cha IFONEO.
Kiemi amesema anapata USHIRIKIANO Mzuri Kutoka kwenye nyuo vingine vya ndani na nje ya nchi. Hata hivyo amesema Ujenzi wa majengo Baadhi Yako tayari , Geti na Fence kuzunguka Eneo lote ni Tayari. Ambapo Kwa Sasa wanamalizia Ujenzi wa Administration Block pamoja na miundombinu mingine Ili Chuo kianze kudahili wanafunzi kufikia mwishoni mwaka 2025.
Kiemi amesisitiza kuwa Watu wa Singida wasiogope kutekeleza mawazo Makubwa na ya muda mrefu yatakayosaidia kufungua macho kielimu ndugu zetu, Majirani na Watanzania wengine wote.
Pia amesema anakaribisha watu wengine au Taasisi Zingine zinazohitaji kushirikiana na Kijiji Cha Nyuki co ltd katika kutekeleza Mradi huu Kwa Ufanisi zaidi.
0 Comments