VAR kufungwa kwa Mkapa

 

sasa waamuzi wa Ligi Kuu Bara wakashusha pumzi kutokana na makosa ambayo wamekuwa wakiyafanya kwenye baadhi ya michezo, baada ya taarifa nje za ujio wa teknolojia ya usaidizi wa video kwa waamuzi (VAR).

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini, Wallace Karia ametoa taarifa hizo njema leo Desemba 16, 2023 katika mkutano mkuu wa shirikisho hilo unaoendelea Iringa.

Karia amefafanua kuwa ufungwaji wa vifaa hivyo utafanywa katika viwanja vinavyokidhi vigezo vya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) na Shirikisho la Mpira wa Miguu Ulimwenguni (FIFA).

“Tumepata VAR ambayo itakuwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa” maneno ya Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments