Wananchi Hanang waomba dawa ziongezwe

Wananchi wa Kijiji cha Jorodom wamevutiwa na jitihada za Serikali zinazoendelea za uelimishaji wa jinsi ya kujikinga na magonjwa ya mlipuko pamoja na usambazaji wa dawa za kutibu maji katika Wilaya ya Hanang mkoani Manyara.

Wakizungumza baadhi ya wananchi wakati wakiendelea kupata elimu hiyo wameomba dawa za kutibu maji ziongezwe ili kukidhi mahitaji.
Mwenyekiti Kijiji cha Jarodom amesema hatua ya serikali kusambaza mabango ya kuelimisha kuhusu kuzingatia kanuni za afya kujikinga na magonjwa pamoja na usambazaji wa mabango ni nzuri katika kuwajali wananchi wake.
“Hii elimu ni nzuri sana maana maana inatupa mwongozo tufanye nini pia kitendo cha kutibu maji mnajali usalama wetu tunataka vidonge zaidi na zaidi “amesema mmoja wa wananchi hao.
Ikumbukwe kuwa Jorodom ni kijiji cha kwanza kuathiriwa na maji ya mafuriko yaliyoambatana na maporoko ya tope ,magogo na mawe hali iliyosababisha vifo na uharibifu mkubwa wa miundombinu ya maji, nyumba na vitu mbalimbali.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments