DODOMA: MBUNGE wa Jimbo la Dodoma Mjini Anthony Mavunde amewataka wanawake wa Dodoma kuchangamkia fursa za kiuchumi zilizopo mkoani hapo ili kujiinua zaidi.
Mavunde ameyasema hayo leo akiongea na wakina mama wajasiriamali wa Dodoma ambao walikuwa wakisheherekea miaka mitatu tangu kuanzishwa kwa US AS ONE-KICOBA
“Ninawapongeza sana kwa muunganiko huu wenye dhamira ya kuinuana kichumi kupitia VICOBA.
“Kwa miaka mitatu tangu kuanzishwa kwenu mmepiga hatua na kupata mafanikio makubwa ikiwemo kuongeza mtaji mpaka kufikia milioni 63,” amesema Mavunde
Amesema, serikali chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan imefanya kazi kubwa ya kuweka mazingira rahisi ya uwekezaji Jijini Dodoma na hivyo kuongeza wigo mpana wa kiuchumi.
“Hivyo nitoe rai kwenu kutumia fursa hii kubwa kushiriki katika shughuli za kiuchumi ili kujiongezea kipato na kukuza uchumi wenu,kama Mbunge wenu nitakuwa tayari kuwashika mkono na kuwaongoza vyema,” amesema
Akisoma risala, Mwenyekiti wa US AS ONE-KICOBA, Pauline Chuma amesema madhumuni yao hivi sasa ni kukua kutoka KICOBA kwenda kuwa SACCOS ili kutanua wigo wa shughuli zao sambamba na kuongeza idadi kubwa ya wanachama ili kuunganisha nguvu kwa pamoja.
Akitoa shukrani kwa niaba, Katibu wa US AS ONE-KICOBA amemshukuru Mavunde kwa kukubali ombi lao la kuwa mlezi wao pamoja na kuwachangia sh milioni3 za ununuzi wa vifaa vya kupikia.
0 Comments