ANZISHENI SHULE MAENEO AMBAYO WANAFUNZI WANATEMBEA UMBALI MREFU KUFUATA SHULE, Meya Manispaa Singida YAGI KIARATU.

 

Meya wa Manispaa ya Singida YAGI KIARATU amewataka viongozi wa Vijiji na Kata kuanzisha shule katika maeneo ambayo wanafunzi wanatembea umbali mrefu kufuata shule ili kuondoa changamoto hiyo inayosababisha Utoro kwa wanafunzi wengi.

KIARATU alisema hayo Changamoto hizo katika Kikao cha Wilaya ya Singida cha Tathmini ya hali ya uandikishwaji wa wanafunzi, Darasa la kwanza na awali, na wale ambao wamefaulu kujiunga na Kidato cha kwanza.

Alisema viongozi wao kama viongozi ni muhimu kutimiza wajibu wao kwa kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wanafunzi hasa suala kukomesha suala la Utoro.

KIARATU pia alisema ni lazima watoto wote wenye sifa za kuanza shule, Darasa la Awali na Darasa la Kwanza wanaandikishwa na wale wanaotakiwa kuripoti kuanza Kidato cha Kwanza ili waweze kupata haki yao ya msingi ya kupata Elimu.

Katibu Tawala Wilaya ya Singida NAIMA CHONDO amewataka wazazi wote ambao hawajawapeleka watoto wao kuwaandikisha shule kuchukuliwa hatua za Kisheria.

Aidha CHONDO alisema sio lazima kwa mwanafunzi kuwa na maCounte Book ili wanze shule kwani uwezo wa wazazi na walezi unatofautiana, hivyo kusiwe na kizuizi hicho.

Hata hivyo inatajwa kuwa Wanafunzi wengi katika Wilaya ya Singida wameshindwa kuripoti shuleni kutokana na changamoto mbalimbali ikiwemo umbali mrefu wa kwenda shule na wazazi kushindwa kumudu baadhi ya mahitaji ya shule.




Na Mwandishi Wetu Lafulu Kinala Singida

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments