AWESO AMPA MKANDARASI SIKU 30 KUKAMILISHA MRADI WA MAJI NAVANGA-MTAMA

 

Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso ametoa siku 30 kwa Mkandarasi Halem Construction kukamilisha ujenzi wa Mradi wa Maji Navanga.


Waziri Aweso ameyasema hayo alipofika Jimbo la Mtama kutembelea na kukagua mradi wa Maji ukanda wa Navanga unaotekelezwa katika kata 5 zilizopo katika Wilaya ya Lindi ambao kwasasa umefikia asilimia 90.

Mradi huu wenye thamani ya Bilion 4.5 utahudumia vijiji hivi vyenye jumla ya watu wapatao 17,015 wenye wastani wa mahitaji ya Maji lita 425,375 kwa siku.

Akihitimisha hotuba yake Waziri Aweso amefikisha salamu za Mbunge wa Jimbo la Mtama Mhe Nape Moses Nnauye aliemuomba kwa dhati kufika Navanga na alieupigania mradi huo kwa dhati mpaka ulipofikia hatua hii ya kukamilika.




TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments