Aweso ataka usimamizi bora mradi wa maji Butimba

WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso ameitaka Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mkoa wa Mwanza (MWAUWASA) kusimamia utaratibu wa kuwaunganishia maji wakazi wa Mwanza na maeneo ya jirani kwani tayari mradi huo wa Butimba umeshakamilika.

Aweso ametoa maelekezo yao mara baada ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kufanya ziara ya ukaguzi katika mradi wa chanzo kipya cha maji cha Butimba jijini Mwanza huku akitoa pongezi kwa Bodi ya Mwauwasa pamoja na uongozi wa Serikali ya Mkoa pamoja na chama kwa usimamizi mzuri wa mradi huo.

Ujenzi wa mradi huo wa chanzo kipya cha maji butimba umefikia asilimia 99 na unatekelezwa kwa gharama ya Sh bilioni 69 na unatarajia kuzalisha lita milioni 48 kwa siku na utahudumua zaidi ya wakazi 450,000.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments