Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akikabidhi
jezi iliyonadiwa kwa wadau wa michezo nchini, wakati alipo mwakilisha Rais,
Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Harambee ya kuchangia timu za taifa
zinazoshiriki michuano ya kimataifa, kwenye ukumbi wa Johari Rotana, jijini Dar
es Salaam, Januari 10.2024, ambapo kiasi cha shikingi bilioni 3.7 zilipatikana.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
#MICHEZO: Siku moja baada ya kupewa mkono wa kwaheri na timu ya Simba Sc, mchezaji kiraka Nassor Kapama amesema huu ni wakati sahihi kwake kuondoka kwenda kujaribu changamoto nyingine nje ya timu hiyo.#BandolaMediaUpdates pic.twitter.com/5jHBRIKxsH
— Bandola Media (@bandolamediatz) January 10, 2024
Fedha hizo zilipatikana kutokana na wadau kutoka sekta mbalimbali ikiwa ni ppamoja na wizara na taasisi za Serikali, taasisi za kifedha, mashirika ya hifadhi za jamii, wafanyabiashara na wasanii pamoja na njia ya mnada ambapo jezi zenye majina ya wachezaji wa timu ya Taifa iliyoshiriki AFCON miaka ya 1980 ziliuzwa na jezi iliyouzwa na gharama kuwa ilikuwa ya golikipa Juma Pondamali iliyonunuliwa kwa shilingi milioni 25.
Mheshimiwa Rais Dkt. Samia ametoa mchango huo jana usiku Jumatano, Januari 10, 2024 wakati alipompigia simu Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwa ajili ya kuzungumza na wadau mbalimbali wa michezo walijitokeza katika hoteli ya Johari Rotana jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuzichangia timu za Taifa.“Wito wangu na ombi langu kwenu Watanzania
wenzangu tuchangie timu zetu ili ziende kuwakilisha vizuri jina la Tanzania.
Serikali imejitahidi na imehamasisha na timu zetu zinasonga mbele, michezo ni
gharama ndugu zangu. Mimi na marafiki zangu kwa kuanzia tutachangia shilingi
milioni 500.
Waziri Mkuu ambaye
aliongoza harambee hiyo kwa niaba ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia alisema lengo
la kukusanya fedha hizo ni kuziwezesha timu za Taifa zinazoshiriki katika
michuano mbalimbali ya kimataifa kusonga mbele. “Serikali ya awamu ya sita
chini ya uongozi thabiti wa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania tumeshuhudia mageuzi makubwa sana katika sekta ya
michezo.”
Baada ya kuhusishwa kujiunga na Young Africans, winga wa timu ya taifa ‘Taifa Stars’, Simon Msuva kwa mara ya kwanza tangu aachane na timu ya JS Kabylie ya Algeria amesema kuwa lolote linaweza kutokea akacheza ligi ya ndani au nje ya nchi.#BandolaMediaUpdates pic.twitter.com/jxS1snT2wJ
— Bandola Media (@bandolamediatz) January 9, 2024
Waziri Mkuu alisema
mageuzi hayo yametokana na jitihada na uwekezaji mkubwa unaofanywa na Serikali
pamoja na wadau mbalimbali yakiwemo makampuni pamoja na watu binafsi, ambapo
utashi mkubwa wa kisiasa katika sekta ya michezo umeleta msukumo chanya unaoongeza
ari na morali kwa wadau wa sekta ya kuunga mkono na kuzienzi jitihada za
Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika uwekezaji na mabadiliko makubwa
katika sekta ya michezo.
Alisema kwa upande wa
mpira wa miguu, Timu ya Taifa ya mpira wa miguu ya wanaume “Taifa Stars”
imefuzu kucheza mashindano ya AFCON yanayofanyika nchini Ivory Coast mwezi huu
Januari 2024. “Ninayo furaha kuwataarifu kuwa hivi sasa timu yetu ipo kambini
nchini Misri na tayari Mheshimiwa Rais amekwisha kutoa fedha za kusaidia Timu ya
Taifa kushiriki mashindano haya.”
Vilevile, Waziri Mkuu
alisema timu ya Taifa ya wanawake ya Mpira wa miguu “Twiga Stars” imefuzu
kucheza mashindano ya WAFCON ambayo yatafanyika mwaka huu nchini Morocco, timu
hiyo nayo imepewa bonasi ya Mheshimiwa Rais ya shilingi milioni 200 ilipofuzu
mashindano hayo.
Awali, Mwenyekiti wa
kamati ya hamasa ya kuchangia timu za Taifa, Bw. Theobaid Sabi alisema kamati
yao ina majukumu makuu matatu ambapo la kwanza ni kutafuta fedha kwa ajili ya
kugharamia timu za Taifa zinazotarajia kushiriki mashindano ya kimataifa,
kuuelimisha umma kuhusu uwepo na umuhimu wa timu za Taifa na kuuhamasisha
kuziunga mkono na kuzichangia timu hizo.
Bw. Sabi ambaye ni
Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya NBC alisema lengo ni kukusanya shilingi bilioni
10, hivyo amewaomba wadau wajitokeze kwa hali na mali kuchangia timu hizo.
Alisema Benki ya NBC itaanza kuchangia shilingi milioni 100.
0 Comments