BUNGE LA REJEA NA MISWADA YA MOTO MINNE MEZANI

Mkutano wa Kumi na Nne wa Bunge la Kumi na Mbili umepangwa kufanyika kwa muda wa wiki tatu kuanzia leo Januari 30 hadi Februari 16, 2024.

Mkutano huo umeongezewa wiki moja kutokana uzito wa majukumu yaliyopangwa ikiwemo uzito wa miswada itakayoshughulikiwa.

Taarifa ya Bunge, inasema miswada ambayo imepangwa kujadiliwa katika mkutano huo ni muswada wa Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani wa Mwaka 2023 na Muswada wa Sheria ya Tume ya Uchaguzi wa Mwaka 2023.

Miswada mingine ni muswada wa Sheria ya marekebisho ya Sheria za Vyama vya Siasa wa Mwaka 2023 na muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na.5) wa Mwaka 2023.

Vilevile katika Mkutano huu wa Bunge Kamati za Kudumu za Bunge zitawasilisha taarifa za shughuli zilizotekelezwa na Kamati kwa mwaka 2023.

Imeelezwa kuwa, wastani wa maswali 250 ya kawaida na maswali 24 ya papo kwa papo yataelekezwa kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, kutoka kwa wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments