Mkuu wa Wilaya ya Tanga, James Kaji amemuagiza Mkurugenzi wa jiji la Tanga, Said Majaliwa kumsimamisha kazi afisa elimu shule za sekondari Lusajo Gwakisa kwa tuhuma za kukiuka muongozo wa serikali katika kusaini mkataba wa ujenzi wa madarasa na majengo ya utawala kwenye shule mpya ya sekondari kiomoni .
Agizo hilo amelitoa mara baada ya kukagua ujenzi wa shule mpya ya sekondari ya kata ya Kiomoni ambayo inatekelezwa kupitia mradi wa SEQUIP ambayo mpaka sasa ujenzi wake haujakamilika.
Ameelekeza kuwa mradi huo unatakiwa ukamilike ifikapo Januari 15 ili wanafunzi waweze kuanza masomo yao katika shule hiyo mpya bila ya changamoto zozote zile
“Nakuagiza mkurungenzi wa jiji msimamishe afisa elimu lakini ajieleze na uchunguzi ufanyike juu ya sababu ya kusaini mikataba ya ujenzi kinyume na taratibu za serikali zilivyoelekeza”amesema DC Kaji.
Hata hivyo Mkurungenzi wa jiji, Saidi Majaliwa amesema kuwa mradi huo upo zaidi ya asilimia 50 ya utekelezaji wake na unatarajiwa kukamilika Januari 15 mwaka huu.
“Hapa sio kwamba kuna uhaba wa madarasa hapana tulikuwa tunaongezea majengo ya utawala na maabara ili watoto waweze kuhamia hapa kutoka shule ya awali na kuendelea na masomo yao katika mazingira mazuri “amesema mkurungenzi huyo.
Amesema kutokana na shule ya awali kuwa na changamoto ya kiafya kutokana na kuwa karibu na eneo la viwanda vya kuzalisha chokaa hivyo waliamua kuhamishia shule katika eneo hilo jipya.
Hata hivyo alisema kuwa kutokana na changamoto hizo gharama za ujenzi wa shule hiyo ziliweza kuongeza kutoka Sh milioni 584 zalizotengwa hadi kufikia zaidi ya Sh milioni 700.
Wananchi wa kata ya Kiomoni wameiomba serikali kuharakisha ujenzi wa shule hiyo ili wanafunzi wasiendele kupata changamoto za kiafya katika shule ya awali.
0 Comments