DC Tanganyika atangaza kiama kwa wazazi

KATAVI: Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi, Onesmo Buswelu ametangaza kiama kwa wazazi wote ambao hadi sasa hawajawapeleka watoto wao waliochaguliwa kuanza masomo ya kidato cha kwanza licha ya shule kufunguliwa Januari 08 mwaka huu.

Akizungumza na wanafunzi wa shule ya Sekondari Kabungu baada ya kikao cha bodi ya shule kilichofanyika katika shule hiyo, Buswelu amesema kufikia jumatatu litatumika Jeshi la akiba kupita kila kona kuwakamata wazazi wote ambao hadi sasa hawajawaachia watoto wao kuanza masomo.

“Kuanzaia Jumatatu ya Januari 15 tutapita kila kona ambayo tunadhani kuwa wanafunzi wako huko, kama ni majarubani tutapita, kama ni kwenye mashamba ya tumbaku tutapita. Tunawataka wazazi wote na walezi wote wawaachie watoto, huu ni muda wao kusoma”

Katika hatua nyingine, DC Buswelu amewataka wakuu wa shule kutomrudisha nyumbani mwanafunzi anayeripoti au kuhamia kisa hana sare za shule wala kumtoza michango ya aina yoyote kwa kuwa hakuna utaratibu wa aina hiyo na tayari serikali imesharuhusu elimu bila malipo na imejenga miundombinu ya kutosha kwa ajili ya kuwahudumia wanafunzi.

“Ni marufuku kwa mwanafunzi anayehamia kutoka shule nyingine kwenda shule nyingine ndani ya Wilaya ya Tanganyika kusema anaongezewa michango eti kwa sababu anahamia pale, shule zote za serikali ni shule ambazo zimejengwa na Rais, Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya wanafunzi na wanayo ruhusa ya kusoma shule yoyote ambayo kwake inampa mazingira rafiki.”

Aidha, ametoa wito kwa wazazi na walezi kutimiza wajibu kwa watoto wao wanaosoma shule ya awali, msingi na sekondari kwa kuwanunulia mahitaji muhimu kama madaftari na kuchangia vyakula.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments