DCEA yatoa mafunzo Arusha

MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Kaskazini imetoa mafunzo kwa asasi za kiraia zinazotoa huduma kwa warahibu juu ya uandishi mzuri wa andiko la miradi likalowasaidia kudhibiti matumizi ya dawa hizo nchini

Mafunzo hayo ya siku moja yamefanyika Arusha na kufunguliwa na Katibu Tawala Msaidizi,Uchumi na Uzalishaji Mali, Hargeney Chitukuro ambaye amesema asasi hizo ziendelee kutoa elimu zaidi na matibabu kwa waraibu wa dawa za kulevya sanjari na umakini wa matumizi ya fedha kwaaajili ya utekelezaji wa kudhibiti matumizi ya dawa hizo nchini.

Amesema uandikaji wa maandiko ya miradi ni muhimu yakazingatia ili kusaidia serikali katika mapambano ya matumizi ya dawa hizo za kulevya sanjari na udhibiti wake kwa kuibua miradi mbalimbali ikiwemo utoaji wa elimu kwa Jamii kuanzia shuleni,vyuoni,taasisi za fedha na nk

Ofisa Maendeleo ya Jamii kutoka ofisi ya DCEA Kanda ya Kaskazini, Sarah Ndaba amesema elimu hiyo ya andishi wa andiko ni muhimu ili kusaidia na wadau hao katika kusaidia Jamii kupata elimu sanjari na ufanyaji kazi kwa ufanisi zaidi na kuisaidia serikali kwenye mapambano hayo.

Mamlaka hiyo inajumla ya asasi zaidi ya 100 na kwa Kanda ya Kaskazini wanaoshirikiana na asasi zaidi ya 16 ambazo zinatoa mrejesho juu ya udhibiti wa dawa hizo sanjari na utoaji mrejesho kwa mamlaka ya DCEA juu ya mchanganuo wa kazi wanazofanya au walizofanya kwa kila mwaka

Naye mmoja kati ya washiriki wa mafunzo hao kutoka Mkoani Tanga kutoka Shirika la Gift of Hope Foundation,Said Bandawe amesema mafunzo hayo ni muhimu kwako kwani yatawasaidia kupata fedha sanjari na kufanya harambee ili kukusanya fedha kwaaajili ya kusaidia shughuli mbalimbali za kudhibiti dawa hizo sanjari na elimu kwa jamii zote.

Wakati huo huo,Ofisa Elimu kutoka DCEA,Shabani Miraji aliongeza kuwa mamlaka hiyo itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali nchini ili kudhibiti dawa hizo sanjari na utoaji elimu zaidi na kubaini mbinu za kudhibiti mbinu mpya wanazotumia wafanyabiashara wa dawa hizo na jinsi ya kuwadhibiti.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments