KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA ARDHI YATEMBELEA KAZI YA UBORESHAJI MFUMO WA SEKTA YA ARDHI

Kamati ya Kudumu ya Bunge Ardhi Maliasili na Utalii imetembelea kazi ya Uboreshaji Mfumo Unganishi wa Usimamizi wa Sekta ya Ardhi inayofanywa na timu ya wataalamu mkoani Arusha.


Mfumo huo unatarajiwa kuanza katika mikoa mitano ya Arusha, Dodoma, Mwanza, Mbeya na Tanga na utarahisisha na kuharakisha upatikanaji huduma za sekta ya ardhi kwa kuwa wananchi watakuwa wakipata huduma kwa njia ya mtandao.

Akizungumza wakati wa kuikaribisha Kamati hiyo jijini Arusha tarehe 8 Januari 2023 Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Jerry Silaa amesema, mfumo unaoboreshwa na timu ya wataalamu mkoani Arusha asilimia mia moja utakuwa ni wa kidigitali.

‘’Baada ya kazi ya maboresho ya mfumo kukamilika, hatua zozote za ardhi zitakuwa zikifanyika kwenye mfumo na suala la mwananchi kwenda ofisi za ardhi kupata huduma ni uamuzi wake mwenyewe’’. Alisema Mhe. Silaa

Mkurugenzi wa Tekonolojia ya Habari na Mawasiliano wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Flateny Hassan ameeleza kuwa, boreshaji wa Mfumo unafuatia Wizara ya Ardhi kuwa na changamnoto kadhaa kwenye mifumo yake jambo alilolieleza kwamba limesababisha kuwepo uhitaji wa kuunganisha mifumo yote ili kuwa na mfumo mmoja utakaohusika na sekta ya ardhi.

‘’Kazi inayofanywa na timu ya wataalmu jijini Arusha kwa sasa imefikia asilimia 85 na matarajio ni kwamba ikifika Juni 2024 mikoa ya awali iliyopangwa itakuwa imefikiwa’’. Alisema Flateny

Maboresho yanayofanyika ni pamoja na mfumo unaoruhusu watumishi wa sekta ya ardhi kutekeleza majukumu yao ndani ya ofisi zao, mfumo unaoruhusu wananchi kuomba huduma kwa njia ya mtanadao na huduma ya Mobile App ambao mwananchi anaweza kupata huduma kupitia njia ya mkononi.

Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi imekuwa katika jitihada kubwa za kuhakikisha huduma za sekta ya ardhi zinapatikna kwa haraka na urahisi kupitia mifumo ya kidigitali.Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Utalii Mhe. Timotheo Mzava akisalimiana na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda alipowasili na timu yake kukagua kazi ya Uboreshaji Mfumo Unganishi wa Usimamizi wa Sekta ya Ardhi inayofanywa na timu ya wataalamu mkoani Arusha. Katikati ni Waziri wa Ardhi Mhe. Jerry Silaa.Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Jerry Silaa akizungumza wakati Kamati ya Kudumu ya Bunge Ardhi Maliasili na Utalii ilipotembelea kazi ya Uboreshaji Mfumo Unganishi wa Usimamizi wa Sekta ya Ardhi inayofanywa na timu ya wataalamu mkoani Arusha tarehe 8 Januari 2023.


Sehemu ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Utalii wakifuatilia uwasilishwaji kazi ya Uboreshaji Mfumo Unganishi wa Usimamizi wa Sekta ya Ardhi inayofanywa na timu ya wataalamu mkoani Arusha.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda akizungumza wakati Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Utalii ilipokwenda jijini Arusha kukagua kazi ya Uboreshaji Mfumo Unganishi wa Usimamizi wa Sekta ya Ardhi tarehe 8 Januari 2024.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii Mhe. Timotheo Mzava akizungumza wakati Kamati yake ilipotembelea kazi ya Uboreshaji Mfumo Unganishi wa Usimamizi wa Sekta ya Ardhi inayofanywa na timu ya wataalamu mkoani Arusha tarehe 8 Januari 2023.
Baadhi ya wataalamu wanaofanya kazi ya kufanya Maboresho Mfumo Unganishi wa Usimamizi wa Sekta ya Ardhi.Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhandisi Anthony Sanga akizungumza wakati Kamati ya Kudumu ya Bunge Ardhi Maliasili na Utalii ilipotembelea kazi ya Uboreshaji Mfumo Unganishi wa Usimamizi wa Sekta ya Ardhi inayofanywa na timu ya wataalamu mkoani Arusha tarehe 8 Januari 2023.Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Jerry Silaa na Naibu wake Mhe. Geophrey Pinda wakifuatilia uwasilishwaji taarifa ya kazi ya Uboreshaji Mfumo Unganishi wa Usimamizi wa Sekta ya Ardhi inayofanywa na timu ya wataalamu mkoani Arusha tarehe 8 Januari 2023.(PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments