Mchezaji huyo ambaye
ameitumikia timu hiyo kwa msimu mmoja na miezi sita, ameiomba klabu hiyo
kumvunjia mkataba ili akajaribu maisha mengine nje ya Simba Sc.
#MICHEZO: Siku moja baada ya kupewa mkono wa kwaheri na timu ya Simba Sc, mchezaji kiraka Nassor Kapama amesema huu ni wakati sahihi kwake kuondoka kwenda kujaribu changamoto nyingine nje ya timu hiyo.#BandolaMediaUpdates pic.twitter.com/5jHBRIKxsH
— Bandola Media (@bandolamediatz) January 10, 2024
Awali, Simba Sc
ilifikia makubaliano ya kutaka kumtoa mchezaji huyo kwa mkopo kwenda Mtibwa
Sugar lakini akagoma na kuomba avunjiwe mkataba ili aweze kwenda timu
anayoitaka akiwa huru.
"Ni kweli
nimepewa barua na Simba Sc ya kunitoa kwa mkopo kwenda Mtibwa Sugar, ila
nimeuomba uongozi tumalizane ili nichague timu ninayotaka kwenda," amesema
mchezaji huyo.
"Kuhusu kuondoka
Simba ilikuwa ni suala la muda kwani nilikuwa sipati nafasi ya kucheza, hivyo
nilihitaji kuondoka ili kwenda kutafuta timu ambayo itanipa nafasi ya
kucheza."
Kapama anasema hadi
sasa upande wake ana ofa kutoka timu sita ambazo ni Ihefu FC, Geita Gold,
Mashujaa Fc, Mtibwa Sugar, JKT Tanzania na Namungo FC.
"Ofa ni nyingi
nimepokea ikiwemo Mtibwa Sugar ambao walitaka kunichukua kwa mkopo kutoka
Simba. Hadi sasa bado sijafanya uamuzi wapi naenda ila kabla ya dirisha
kufungwa nitasajili timu ambayo itanipa ofa nzuri," anasema.
Tangu alipotua Simba Sc, Kapama amecheza zaidi ya mechi 10 za mashindano ilizocheza timu hiyo ikiwemo Kariakoo Derby timu hiyo iliposhinda mabao 2-0 msimu uliopita.
0 Comments