Klopp Kuachana Na Liverpool Mwishoni mwa Msimu Huu.

BREAKING: Kocha wa Liverpool, Jürgen Klopp ametangaza kujiuzulu nafasi hiyo mwishoni mwa msimu huu.

Baada ya kuiongoza ‘The Reds’ kwenye fainali nyingine ya Carabao Cup dimba la Wembley Jumatano usiku, Klopp ,56, ataendelea kusimamia mechi zilizosalia za timu hiyo msimu huu.

Wasimamizi wasaidizi Pepijn Lijnders na Peter Krawietz, pamoja na mkufunzi wa maendeleo, Vitor Matos, pia wataacha nyadhifa zao mwishoni mwa msimu huu, huku Lijnders akitaka kuendeleza taaluma yake ya usimamizi.

Alisema: “Naelewa kuwa ni mshtuko kwa watu wengi wakati huu, unapoisikia kwa mara ya kwanza, lakini ni wazi naweza kuielezea au angalau kujaribu kuielezea.

“Napenda kila kitu kuhusu klabu hii, napenda kila kitu kuhusu jiji, napenda kila kitu kuhusu wafuasi wetu, napenda timu, napenda wafanyakazi. Ninapenda kila kitu. Nachukua uamuzi huu kuonesha kuwa ndio ninalazimika kuchukua.” Amesema Klopp.

Klopp aliteuliwa kuwa meneja wa Liverpool mnamo Oktoba 8, 2015. Ulikuwa uamuzi ambao ungebadilisha klabu na kuifanya kuwa tishio ndani na nje ya England.

Chini ya usimamizi wake, Liverpool wamenyanyua UEFA Champions League, Premier League, FIFA Club World Cup, FA Cup, League Cup na UEFA Super Cup, pamoja na FA Community Shield.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments