Ladack Chasambi ameanza Mazoezi Mepesi yakujiweka Fiti kabla ya Mazoezi ya Jumla siku ya Kesho, Chasambi ametambulishwa Leo Kujiunga na Wekundu wa Msimbazi akitokea Mtibwa Sugar ya Morogoro.
Ladack Chasambi katika tizi jepesi kabla ya kesho kuanza mazoezi rasmi. #UchumiWaBuluu #VisitZanzibar #WenyeNchi #NguvuMoja pic.twitter.com/Z4hq0617zq
— Simba Sports Club (@SimbaSCTanzania) January 8, 2024
Zaidi,
Simba Sc imeendelea kuweka salama malengo yao ya kuchukua taji la pili msimu
huu ikitinga hatua ya nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi baada ya kuichapa
Jamhuri ya Pemba kwa bao 1-0.
Matokeo
hayo sasa yanaifanya Simba Sc kuifuata Singida Fountain Gate ambao mapema jioni
ilitangulia nusu fainali baada ya kuichapa Azam Fc kwa mabao 2-1.
Goli la ushindi dhidi ya Jamhuri SC. #MapinduziCup2024 #UchumiWaBuluu #VisitZanzibar #WenyeNchi #NguvuMoja pic.twitter.com/NgE9hvSvoG
— Simba Sports Club (@SimbaSCTanzania) January 8, 2024
Simba Sc haikuwa na dakika 90 rahisi mbele ya Jamhuri kama ambavyo ilikuwa ikidhaniwa kwani vijana hao wa Pemba walikuja na akili tofauti na mbinu na kuwabana vizuri wekundu hao kwa muda mwingi wa mchezo huo.
0 Comments