Mabasi kutoka Arusha kwenda mikoani kuwa na tiketi mtandao

MENEJA wa Mamlaka ya Udhibiti na Usafiri Ardhini (LATRA) Mkoa wa Arusha, Michael Joseph amewataka wamiliki wa vyombo vya usafiri vinavyotoka nje ya jiji hilo kuhakikisha wanakata tiketi mtandao kwa abiria vinginevyo hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.

Michael Joseph amesema hayo leo jijini Arusha wakati wa usimamizi wa utekelezaji wa agizo la serikali la kusitisha leseni za mabasi 35 ya Kampuni ya Kilimanjaro Truck na kuhakikisha nauli za abiria zinarudishwa na kampuni hiyo.

Alisema kila abiria aliyekata tiketi za karatasi katika mabasi ya Kilimanjaro Truck anapaswa kurudishiwa nauli na abiria wameambiwa kuwa lazima na wao wakata tiketi mtandao kwa maslahi ya serikali na kuanzia leo mabasi hayo hayatafanya usafiri wa kusafirisha abiria sehemu yoyote ya nchi.

Meneja alisema mmiliki wa Kilimanjaro Track amekuwa msumbufu kwa abiria kwa kushindwa kutekeleza agizo la serikali na kufanya maofisa wa Latra kote nchini kuingia barabarani na kuhakikisha kampuni hiyo haifanyi kazi na pia kuhakikisha wale wote waliokata tiketi karatasi wanarudishwa nauli.

‘’Serikali imeshatoa agizo kwa kampuni ya Kilimanjaro Truck kusitisha kutoa huduma ya usafiri kuanzia leo hadi atakapotelekeza agizo la serikali na kuhakikisha inarudisha nauli za abiria’’

‘’Abiria tunaomba kila mmoja ahakikishe anakata tiketi mtandao kwa ajili ya safari kwa kila basi linalotoka nje ya mkoani Arusha ili kuondoa usumbufu usiokuwa wa lazima.” alisema Joseph

NKamanda wa Polisi wa Kikosi cha Barabarani mkoani, Arusha Zauda Mohamed alisema kuwa kila mmiliki wa mabasi ya usafiri mkoani humo anapaswa kufuata taratibu zilizowekwa na serikali ikiwa ni pamoja na kutoa tiketi mtandao kwa abiria na kuacha mara moja kuongeza nauli kwani ni kinyume na taratibu.

Kamanda huyo pia amesisitiza kwa madereva wa mabasi hayo kufuata ratiba iliyopangwa na mamlaka husika ili kuondoa sitofahamu zisizo za lazima kwa abiria kwa kuondoka kituoni bila kufuata utaratibu kwani kunaweza kuleta usumbufu usiokuwa wa lazima.

‘’Niko hapa toka alfajili kuhakikisha kila abiria anarudishiwa nauli katika mabasi ya Kilimanjaro na abiria wengine kuwahimiza kukata tiketi mtandao kwani serikali ilishatoa maagizo hayo’’alisema kamanda wa barabarani Arusha

Januari 6 mwaka huu Mkurugenzi Mkuu wa Latra, Habibu Suluo alisitisha leseni na ratiba za mabasi 35 ya Kilimanjaro Truck baada ya kujilidhisha kuwa mtoa huduma huyo ameendelea kukiuka sheria ,taratibu na kwa makusudi na hata baada ya kutembelewa ,kushauriwa na kuelekezwa kwa barua.

Suluo alisema kuwa Mamlaka iliutangazia umma kuwa imesitisha leseni na ratiba za mabasi 35 ya kampuni ya Kilimanjaro kuanzia leo januari 8 mwaka hu una kampuni hiyo itaruhusiwa kurejesha huduma za mabasi yake baada ya kuwa na mfumo wa tiketi mtandao kuingiza nauli zisizozidi viwango vilivyoidhinishwa na Latra kwenye Mfumo na kuwasilisha maombi yatakayoridhiwa Latra.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments