Simba Sc imemtambulisha nyota mwingine wa kimataifa kutoka nchini Ivory Coast, Freddy Michael Kouablan akitokea klabu ya Green Eagles ya Zambia.
Mshambuliaji huyo amesaini mkataba wa miaka
miwili kutumika Simba katika kuimarisha safu ya ushambuliaji ambayo.Kocha Mkuu
wa timu hiyo, Abdelhak Benchikha akihitaji kuongezewa mshambuliaji.
Katika mkatana huo, inaelezwa kuwa Freddy
atakuwa analipwa mshahara wa Dola 6500 sawa na Milioni 16.25 kwa mwezi, huku
akihakikishiwa usafiri na nyumba ya kuishi nnje ya kambi ya timu.
Kouablan hadi sasa ndiye anaongoza kwa
ufungaji kwenye ligi kuu ya Zambia kwa kuweka kambani mabao 14 na assist 4
katika michezo 17 aliyocheza.
Usajili wa nyota huyo umekuja saa chache
baada ya kutangaza mshambuliaji mwingine Pa Omar Jobe akitokea katika klabu ya
FC Zhence inayoshiriki Ligi Kuu nchini Kazakhstan.
Ujio wa nyota hao unazidi kuhatarisha
nafasi za washambuliaji wawili wa Simba, Jean Baleke na Mosses Phiri kuendelea
kutumikia kikosi cha kwanza cha timu hiyo.
Hata hivyo inafahamika kuwa Jean Baleke atajiunga na FC Goliath ya Bangladesh, huku Moses Phiri yeye ikiwa bado haijajulikana ataenda klabu gani japo vyanzo vyetu vya habari vinadai kuwa huenda akarudi kwao Zambia.
0 Comments