Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda ameingia uwandani kutatua na kufuatilia utekelezaji wa maagizo yake ya migogoro ya ardhi katika jiji la Dodoma.
#HABARI: Mbunge wa jimbo la Ushetu, Mhe. Emannuel Cherehani amewataka wananchi kutumia uwepo wa umeme wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kujiletea maendeleo ya kiuchumi.-https://t.co/ty9lFDEwan pic.twitter.com/ktwE83f8wY
— Bandola Media (@bandolamediatz) January 12, 2024
Naibu Waziri wa Ardhi alianza ziara yake kwa kutembelea eneo la Chang'ombe Mbwanga ambapo Bi Dorothy alibomolewa kimakosa ukuta wa nyumba yake na halmashauri ya jiji la Dodoma ambapo Mhe. Pinda alielekeza mwananchi huyo kujengewa ukuta huo.
‘’Ninyi mnaoishi hapa sura ya ujirani lazima itengenezwe kwa kuepuka migogoro ya ardhi katika maeneo yenu, mnataka mpaka waziri aje ndiyo atengeneze ujirani’’ alisema Mhe. Pinda
Aidha, alitembelea eneo la Chang'ombe Extension, ambapo mwananchi mmoja Ramadhani Kisiju anadai kumiliki kiwanja alichokuwa akilima kwa muda mrefu.
Katika kutafuta suluhu ya eneo hilo, Mhe Pinda aliagiza mmiliki wa eneo analodai Kisiju kumiliki afiki ofisini kwake na nyaraka zote za umiliki kwa lengo la kupata muafaka wa mgogoro huo.
‘’Kitu kimoja ninachotaka kukusaidia mzee wangu, ngoja tukaangalie hiki kiwanja uhalali wake halafu baadaye tutakupa majibu’’ alisema Naibu Waziri wa Ardhi.
Uamuzi wa Mhe Pinda kutembelea na kukagua maeneo ya mgogoro uwandani unafuatia kuwasilishwa kwa malalamiko ya migogoro ya ardhi kwake huku baadhi ya malalamiko yakihusisha watendaji wa sekta ya ardhi.
#HABARI: Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda ameingia uwandani kutatua na kufuatilia utekelezaji wa maagizo yake ya migogoro ya ardhi, Msikilize Hapa -https://t.co/gKMRaRQgBG pic.twitter.com/fFV2SFGCqU
— Bandola Media (@bandolamediatz) January 12, 2024
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda akizungumza na wananchi aliowakuta kwenye eneo lenye mgogoro Chang’ombe Extensition jijini Dodoma wakati alipokwenda kutatua mgogoro wa ardhi tarehe 11 Januari 2024. (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)
0 Comments