Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) wamekutana na kufanya kikao cha pili cha baraza la pili wakiongozwa na Mkurugenzi Mkuu Dkt. Erasmus Kipesha. Kikao hicho kilifanyika Januari 19, 2024 Mjini Morogoro.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Dkt. Erasmus Kipesha akizungumza na wajumbe wa Baraza la wafanyakazi alipokuwa akifungua kikao cha pili cha Baraza la wafanyakazi wa Mamlaka hiyo mjini Morogoro
Mwakilishi kutoka Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi ya Elimu ya juu Tanzania (THTU) Taifa Bi. Salma Fundi, akiwasilisha salamu kutoka makao makuu ya chama hicho kwa wajumbe wa Baraza la wafanyakazi wa TEA.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Dkt. Erasmus Kipesha akifafanua jambo katika kikao cha pili cha Baraza la wafanyakazi wa Mamlaka hiyo kilichofanyika mjini Morogoro.
Baadhi ya wajumbe wa Baraza la wafanyakazi la TEA wakisikiliza na kufuatilia taarifa mbalimbali zikiwasilishwa katika kikao cha pili cha Baraza hilo kilichofanyika mjini Morogoro.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Dkt. Erasmus Kipesha (Katikati) akisikiliza na kufuatilia taarifa mbalimbali katika kikao cha Baraza la Wafanyakazi kilichofanyika mjini Morogoro. Kushoto ni Katibu wa Baraza hilo kutoka TEA Bw.Aidan Lucas .
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Dkt. Erasmus Kipesha katika picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza la wafanyakazi wa Mamlaka hiyo mjii Morogoro.
0 Comments