Ambao wanatuhumiwa kuhusika na mauaji ya
Sophia Maduka,(61) na Mathias Lusesa,(73) wote wakulima na wakazi wa Lwenge
Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza.
Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Mwanza Wilbroad Mutafungwa ameeleza kuwa mnamo Oktoba 12,2023
majira ya saa mbili (20:00) usiku katika Kijiji cha Lwenge Kata ya Kagunga
Wilaya ya Sengerema watu wawili waliuawa kwa kukatwa na vitu vyenye ncha kali
sehemu mbalimbali za miili yao.
Mutafungwa ameeleza kuwa baada ya taarifa
hiyo kuripotiwa kituo cha polisi,jeshi hilo lilifanya msako mkali na kufanikiwa
kuwakamata watuhumiwa hao waliokuwa wamejificha kukwepa mkono wa sheria.
Ambapo Januari 06,2024 kwa nyakati tofauti
na maeneo tofauti katika Mkoa wa Geita na Shinyanga Askari wa upelelezi kutoka
Mkoa wa Mwanza kwa kushirikiana na Askari wa mikoa hiyo jirani walifanikiwa
kuwakamata watuhumiwa hao watano.
Mutafungwa amewataja watuhumiwa hao kuwa ni
Selina Mchele(48),mkulima na mkazi wa Kijiji cha Mwakilemwa,Maneno
Mashauri,(19)mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya sekondari Lwenge
Wilaya ya Sengerema, Majaliwa Damas,(22) Mganga wa tiba asilia,mkazi wa
Masumbwe mkoani Geita, Ntingwa Kilimanjaro kwa jina maarufu Shetani(42)mkulima
na mkazi wa Kijiji cha Mbamba mkoani Geita na Emmanuel Damas,(34),Mganga wa
tiba asilia,mkazi wa Kijiji cha Burungwa mkoani Shinyanga.
0 Comments