MWENEZI MAKONDA AFIKA OFISI ZA MKUU WA MKOA WA SINGIDA KUKAGUA UTEKELEZAJI WA AGIZO LA CCM

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndugu. Paul Makonda amefika katika Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Singida kukagua agizo la Chama Cha Mapinduzi alilolitoa jana tarehe 25 kwenye Mkutano wa hadhara Mkoani Singida la kumtaka Mkuu wa Mkoa wa Singida na Wakuu wake wa Wilaya kuanzisha Kliniki za kusikiliza kero mbalimbali na kuzitatua siku hiyohiyo kwa zile ambazo hazina mlolongo mrefu ilikusudi kuondoa maumivu yaliyo miyoyoni mwa Watanzania.

Mwenezi Makonda yupo mkoani Singida ambapo anatarajia kuelekea Mkoani Tabora kwa muendelezo wa ziara yake ya Mikoa

>

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments