Waziri wa Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba (Mb) akizungumza na
Balozi wa India nchini Mhe. Binaya Srikanta Pradhan aliyefika katika Ofisi
ndogo za Wizara jijini Dar es Salam kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa
uwakilishi nchini.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba (Mb) akizungumza na Balozi wa India nchini Mhe. Binaya Srikanta Pradhan aliyefika katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salam kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa uwakilishi nchini.
Balozi wa India nchini Mhe. Binaya Srikanta Pradhan akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba (Mb) alipofika katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salam kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa uwakilishi nchini.
Akizungumza katika
kikao hicho kilichofanyika katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salam
tarehe 10 Januari, 2024, Mhe. Waziri Makamba amemshukuru Mhe. Binaya kwa
jitihada zake za kuhakikisha uhusiano kati ya Tanzania na India unakua na
kuimarika.
Amempongeza pia kwa mafanikio yaliyopatikana kupitia ziara iliyofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan nchini India na kufanikisha kusainiwa kwa Hati za Makubaliano ya Ushirikiano wakati wa ziara hiyo.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba (Mb) na ujumbe wake (kulia) akizungumza na Balozi wa India nchini Mhe. Binaya Srikanta Pradhan na ujumbe wake (kushoto) walikutana katika Ofisi ndogo za wizara jijini Dar es Salam.Waziri wa Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba katika picha na Balozi
wa India nchini Mhe. Binaya Srikanta Pradhan alipofika katika Ofisi ndogo za
Wizara jijini Dar es Salam kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa uwakilishi
nchini.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki Mhe. January Makamba akimkabidhi zawadi ya picha ya Balozi wa
India nchini Mhe. Binaya Srikanta Pradhan alipofika katika Ofisi ndogo za
Wizara jijini Dar es Salam kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa uwakilishi
nchini.
Naye Mhe. Balozi Binaya ameshukuru kwa ushirikiano alioupata kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Serikali kwa ujumla wakati wote wa kipindi chake alichohudumu nchini.
0 Comments