#HABARI: Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Mwinyi amekubali ombi la kujiuzulu la Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale, Simai Mohammed Said, kuanzia leo January 26, 2024 ikiwa ni saa chache baada ya Simai kutangaza kujiuzulu a kutekeleza jukumu hilo yamekuwa magumu. #BandolaMediaUpdates pic.twitter.com/GxA4WrkOGU
— Bandola Media (@bandolamediatz) January 26, 2024
Simai alinukuliwa
akisema “Nimeandika barua kwenda kwa Rais Dkt. Mwinyi ya kujiuzulu kuanzia leo,
nimefikia uamuzi huu ambao hapa kwetu sio rahisi katika utamaduni wetu kutokana
na imani yangu kwamba jukumu namba moja la Wasaidizi wa Rais wakiwemo Mawaziri
ni kumsaidia kutekeleza Ilani ya Chama na inapotokea mazingira yasiyo rafiki
katika kutekeleza jukumu hilo muhimu kwa ustawi wa Wananchi ni vema kutafuta
jawabu kwa haraka ili kazi ya kuwaletea Wananchi maendeleo iweze kuendelea na
hata ikibidi kukaa pembeni”
“Mimi nimefikia
uamuzi huo mgumu wa kukaa pembeni, namshukuru Rais kwa kuniteua, nitaendelea
kuwa Mtiifu kwa Serikali na CCM wakati wote nitakuwa tayari kutoa ushauri wowote
utakaohitajika kwa Serikali ili kuhakikisha Ilani ya Chama chetu inatekelezwa
kwa uaminifu” — Simai.
0 Comments