RITA YAENDELEA KUTOA ELIMU UMUHIMU WA KUANDIKA WOSIA

 WAKALA wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) umewataka wa wananchi kufika kwenye banda lao lililopo katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam ambako kunafanyika Maonesho ya wiki ya Sheria.

Akizungumza katika viwanja hivyo, Ofisa Sheria wa RITA Bestina George amesema wameungana na Mahakama katika viwanja hivyo na watajikita kutoa elimu ya usajili wa vizazi, vifo, ndoa , talaka na usajili wa bodi ya udhamini.

Pia watatoa elimu jinsi ya kuasajili uasili wa watoto huku akieleza pia wanatoa  elimu ya wosia katika kuandika na kutunza na kwamba katika wosia wanatoa elimu kuhusu wosia, kutunza wosia, nani anastahili kuandika na vitu gani muhimu vinatakiwa kuwepo kwenye wosia .
Ameongeza wanatoa bei elekezi za wosia huku akisisitiza wosia ni muhimu sana ,hivyo ni vema wananchi wakafika kupata  elimu ya kuandika wosia kwani ukiuandika unaiacha familia yako ikiwa mikono salama.

“Ugomvi na mivutano katika mali inakuwa haipo na bei zetu za kuandika wosia ni rahisi sana.Mali inayoanzia thamani ya Shilingi moja mpaka Sh.milioni  50 bei ya kuandika ni 20,000 na kutunza Sh.20000.

“Kama mali ni thamani ya Sh.milioni 51 mpaka Sh.milioni 200 kuandika wosia ni Sh.50,000 na kutunza Sh.50,000 wakati mali ya thamani ya milioni Sh.milioni 201 mpaka Sh.milioni 500 kuandika ni 100,000 na kutunza ni 100,000.”

Ameongeza mali inayoanzia thamani ya Sh.milioni  501 na kuendelea kuandika ni Sh.150,000 na kutunza ni Sh.150000 huku akifafanua kufanya marekebisho ya wosia bei ni ile ile kama ni thamani ya Sh.20,000 basi marekebisho yatakuwa ya bei hiyo hiyo.

“Tunatoa elimu ya mirathi ambayo nayo imekuwa changamoto kubwa , kwa hiyo tunaelekeza wananchi njia gani wanaweza kutumia ili RITA tuweze kusimamia mirathi yao, wananchi wengi hawana elimu kwamba RITA tunaweza kusimamia mirathi yao wanapokuwa na changamoto.

“Kwa hiyo RITA tunawapa elimu wananchi kuhusu njia za kufuata ili tuweze kusimamia mirathi hiyo.Pia tunatoa elimu kuhusu bodi ya wadhamini kwasababu sasahivi tumeingia kwenye mfumo na kila kitu tunafanya kwenye mfumo…
“Kwahiyo tunawapa elimu jinsi gani watafanya marejesho ya wadhamini, jinsi gani watafanya wanapotaka kubadilisha wadhamini, jinsi gani watafanya wanapotaka kubadilisha anuani.

“Wanapotaka kumiliki kiwanja kwasababu lazima hatilimiliki itoke kwa kabidhi wasihi mkuu, kwa hiyo tunaelekeza njia zote wanazotakiwa kufanya ili wafanikiwe,”amesema.

Aidha amesema wanatoa elimu jinsi gani wanaweza kusajii bodi ya wadhamini na kwamba katika banda lao la RITA wanatoa usajili wa vizazi na vifo kwani kama inavyofahamika wameanza kutoa huduma zao tandaoni.

Amesema kwa hiyo wanaelekeza wananchi jinsi gani ya kufanya maombi mtandaoni na nyaraka gani muhimu mhusika anatakiwa kuwa nazo ili afanye maombo ya kupata cheti za kuzaliwa au kifo.

“Ili kufanikisha maombi hayo mteja anatakiwa kuwa vitu viwili kati ya hivi nitakavyotaja, kadi ya kliniki, tangazo , chetu cha nasaba unasaba, cheti za ubatizo, cheti cha elimu ya sekondari , kitambulisho cha kura au kitambulisho cha NIDA
“Lakini kuna cheti za kuzaliwa , tunamshauri mteja aende shuleni kuandikiwa barua yenye tarehe ya kuzaliwa na shule alimaliza lini.Kama mteja hana basi anatakiwa kuambatanisha kitambulisho cha mzazi wake au barua ya mtendaji wa kijiji.”

Kuhusu upande wa usajili wa vifo amesema wanatoa elimu kuhusu nyaraka muhimu ambazo mteja anatakiwa kuwa nazo ili afaniwe maombi yake.Kifo cha hospitalini awe na kibali cha mazishi .

Wakati kifo cha nyumbani anatakiwa kuwa na barua kutoka kwa mtendaji wa kata au kijiji ambapo mtendaji atathibitisha kwamba terehe fulani mwaka fulani kuna mwananchi alifariki katika kijiji chake.

Mteja akishafanya maombi mtandaoni, pale cheti kinapokuwa tayari tunamjulisha katika akaunti yake ili afuate cheti chake.Kwahiyo niwakaribishe wananchi wote mkaribie katika banda la RITA mpate elimu kuhusu huduma tunazozitoa.”



TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments