Sekondari Njombe yavunja rekodi udahili wa wanafunzi

IDADI ya udahili wa wanafunzi katika shule ya sekondari ya Bweni ya Yakobi iliyoko mkoani Njombe imeongezeka kutoka wanafunzi 105 hadi kufikia 433 mwaka huu.

Akizungumza leo Mkuu wa shule hiyo, Editor John amesema ongezeko hilo limesababishwa na jitihada za serikali katika kuongeza mabweni shuleni hapo.

Akifafanua alisema, jumla ya Sh milioni 543 zilipelekwa na serikali kwa ajili ya upanuzi wa miundombinu ya elimu kwa ajili ya kidato cha tano na sita ambapo fedha hizo zimeweza kujenga mabweni matatu ya watoto wa kike, madarasa matano pamoja na matundu 14 ya vyoo.

“Tulifanikiwa kutekeleza ujenzi wa mabweni matatu ambayo yamekamilika na wanafunzi wanaishi, madarasa matatu, ofisi moja, matundu 16 badala ya 14 pamoja na samani za ndani ya mabweni ambapo ilitakiwa kununua vitanda vya deka 120 lakini kupitia matumizi mazuri ya fedha hizo, vilinunuliwa vitanda vya deka 180 na badala ya kununua viti 200 na meza 200, imewezekana kununua viti 380 na meza 380,” amesema Editor.

Aidha alisema, mwezi Agosti, 2023 serikali iliwapa tena jumla ya Sh milioni 130 kwa ajili ya ujenzi wa bweni lingine la wasichana ambalo linakaribia kukamilika.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments