Serukamba Atoa Siku 6 Mbegu Za Alizeti Kufika Kwa Wananchi Halmashauri Zote Mkoani Singida

Mkuu wa Mkoa wa Singida PETER SERUKAMBA amewataka Viongozi wa Halmashauri zote za Mkoa huo, kuhakikisha Mbegu za Alizeti zenye Ruzuku, zinasambazwa kwa wakulima, na endapo muda huo utapita, zitarudishwa kwa Wakala wa Mbegu -ASA.

 SERUKAMBA alitoa agizo hilo katika Kikao kazi cha Mkuu wa Mkoa wa Singida, Viongozi wa Mkoa, Wilaya na Halmashauri zote Mkoa huu, kikao ambacho kilijadili Agenda mbalimbali za maendeleo ya Mkoa huo.

 Alisema hakuna sababu ya mbegu hizo kubaki kwenye Maghala kama hazitawafikia wakulima ni bora Wakala wa Mbegu - ASA azipeleke mikoa mingine ambayo inauhitaji wa Mbegu za Alizeti.

 SERUKAMA aliwataka Viongozi wa Halmashauri zote na Maafisa Ugani kutumia siku Sita (6) kuhakikisha Mbegu hizo sinasambazwa na kuwafikia wakulima katika Msimu huu wa Kilimo.

 Baadhi ya wajumbe wa Kikao Kazi hicho walisema ni vyema kuutumia Msimu huu wa Kilimo kubaini changamoto zilizojitokeza katika Misimu iliyopita ili kuzitatua kwa ajili ya misimu ijayo ya kilimo.

 Walisema endapo changamoto hizo zitatuliwa, na Begu zikawafikia wakulima kwa wakati itasaidia wakulima wengi kuzalisha kwa tija na kuongeza vipato vya familia zao na Taifa kwa ujumala.

 Hata hivyo baadhi ya wajumbe walisema bado kuna changamoto ya Bei kubwa ya Begu ya Alizeti, hali inayosababisha wakulima wengi kushindwa kumudu Bei hizo na kuenedelea kutumia mbegu za kienyeji.





TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments