Stawavumilia Viongozi Wanaoshidwa Kusimamia Miradi ya Maendeleo


           
Mkuu wa Mkoa wa Singida PETER SERUKAMBA amesema hatowavumilia Viongozi wa Manispaa ya Singida wanaoshindwa kusimamia Ujenzi wa Miradi ya maendeleo na kusababisha Miradi hiyo kutokumaliza kwa wakati.

Serukamba  alitoa kauili hiyo  wakati akikagua Mirada ya Hospitali ya Manispaa na Jengo la Ofisi Mpya za Singida Manispaa ambapo alibaini ujenzi wa Jengo la Utawala la Manispaa hiyo kusuasua kutokana na baadhi ya viongozi kutokusimamia mradi huo kikamilifu.

Serukamba alisema Halmashauri zinatakiwa kutafuta mafundi wa uhakika ili kumaliza kazi kwa wakati na kutekeleza miradai ya maendeleo kwa munda uliopangwa.

Aidha Mkuu wa mkoa wa Singida Peter Serukamba amesema kuwa wanatakiwa kununua vifaa kwa wakati ili kuweka urahisi wa kazi katika miradi mbalimbali ya maendeleo kwa manufaa ya jamii na taifa kwa ujumla.SITAWAVUMILIA VIONGOZI WANAOSHINDWA KUSIMAMIA MIRADI YA MAENDELEO ASEMA PETER SERUKAMBA

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments