Wananchi wenzangu baada ya salamu za Mwaka Mpya napenda kuwafahamisha
kuwa Kamati ya Mfuko wa Jimbo (Mfuko wa Mbunge) ambayo Mwenyekiti ni Mbunge
iliyoketi tarehe 04.01.2024 iliweza kujadili maombi ya miradi ya wananchi
kutoka Kata Kumi na tatu( 13) na baada ya kikao kamati ilitenga fedha kiasi cha
Sh 67,498,970 katika miradi hiyo kwa mchanganuo kama ifuatavyo;
ISOME NA HII - Tanzania nafasi ya pili uzalishaji tumbaku 2022/2023
1. Pesa kwa ajili ya Kusaidia ujenzi wa
vyoo vya shule ya Msingi ya Sambaru katika Kata ya Mang’onyi,Kijiji cha Sambaru
kiasi cha Sh 2,000,000.
2. Pesa kwa ajili ya Kusaidia ukamilishaji
wa ujenzi wa matundu ya vyoo Shule ..ya msingi Mwau Kata ya Mang’onyi,Kijiji
cha Mwau kiasi cha Sh 2,000,000.
3. Pesa kwa ajili ya Kusaidia umaliziaji wa
ujenzi wa nyumba ya mwalimu Shule ya Msingi Choda Kata ya Mkiwa,Kijiji cha
Choda kiasi cha Sh 2,000,000.
#SINGIDA: Wananchi wenzangu wa Jimbo la Singida Mashariki nachukua fursa hii kuwatakia Kheri ya Mwaka Mpya 2024.Namwomba Mwenyezi Mungu awape Baraka, Afya Njema na Neema katika mwaka huu 2024.#BandolaMedia pic.twitter.com/hqAJBnfm6w
— Bandola Media (@bandolamediatz) January 9, 2024
4. Pesa kwa ajili ya Ujenzi wa Kituo cha
Polisi Kata ya Mkiwa,Kijiji cha Mkiwa Sh 5,000,000.
5. Pesa kwa ajili ya Ujenzi wa matundu ya vyoo
Shule ya Sekondari Mkunguwakihendo Kata ya Kikio Kiasi Sh 2,000,000.
6. Pesa kwa ajili ya Kusaidia ujenzi wa
madarasa Shule Shikizi ya Mwitumi Kata ya Kikio,Kijiji cha Nkundi kiasi cha Sh
10,000,000.
7. Pesa kwa ajili ya Kusaidia ujenzi wa
Shule ya Utayari katika shule shikizi ya Kinyaghimbi Kata ya Ikungi Kijiji cha
Matongo kiasi cha Sh 3,000,000.
8. Pesa kwa ajili ya Ununuzi wa samani za
ofisi Shule ya Msingi Mbughantigha Kata ya Ikungi,Kijiji cha Matongo kiasi cha
Sh 1,000,000.
9. Pesa kwa ajili ya Ununuzi wa mashine ya
kudurufu (Photocopy Machine),Shule ya Msingi Matongo Kata ya Ikungi katika
Kijiji cha Matongo kiasi cha Sh 3,000,000.
10. Pesa kwa ajili ya Ununuzi wa Printer
Shule ya Sekondari Matongo Kata ya Ikungi ,Kijiji cha Matongo kiasi cha Sh
1,000,000.
11 .Pesa kwa ajili ya Umaliziaji wa darasa
na ukarabati wa kisima cha maji Shule ya Msingi Tumaini Kata ya Issuna,Kijiji
cha Tumaini kiasi Sh 2,000,000.
12. Pesa kwa ajili ya Kusaidia ujenzi wa
madarasa Shule Shikizi Muve Kata ya Mungaa,Kijiji cha Kinku kiasi cha Sh
5,000,000.
13.Pesa kwa ajili ya Kusaidia ujenzi wa
matundu ya vyoo Shule ya Msingi Kimbwi Kata ya Makiungu,Kijiji cha Kimbwi kiasi
cha Sh 1,500,000.
14.Pesa kwa ajili ya Kusaidia ujenzi wa madarasa Shule ya Msingi
King’inga Kata ya Unyahati,Kijiji cha Ulyampiti kiasi cha Sh 1,500,000.
15.Pesa kwa ajili ya Kusaidia ukarabati wa vyumba vya madarasa 2 na choo cha wanafunzi Shule ya Msingi Kinyamwandyo Kata ya Unyahati,Kijiji cha Kinyamwandyo kiasi cha Sh 2,000,000.
16.Pesa kwa ajili ya Kusaidia ujenzi wa
matundu ya vyoo katika Zahanati Kata ya Dung’unyi, Kijiji cha Samaka kiasi cha
Sh 1,500,000.
17.Pesa kwa ajili ya Kukarabati Ofisi ya Mtendaji wa Kata ya
Siuyu,Kijiji cha Siuyu kiasi cha Sh 3,000,000.
18.Pesa kwa ajili ya Kusaidia ujenzi wa madarasa 2 Shule Shikizi ya
Msui Kata ya Misughaa,Kijiji cha Msule kiasi cha Sh 2,000,000.
19.Pesa kwa ajili ya Kusaidia ujenzi wa Zahanati Kata ya Ntuntu,Kijiji
cha Mampando kiasi cha Sh 1,498,970.
20.Pesa kwa ajili ya Kusaidia ujenzi wa madarasa Shule Shikizi ya
Sanya Kata ya Lighwa,Kijiji cha Lighwa Kiasi cha Sh 3,000,000.
21.Pesa kwa ajili ya Kusaidia ujenzi wa
maabara Shule ya Sekondari ya Lighwa Kata ya Lighwa,Kijiji cha Mwisi Kiasi cha
Sh 2,000,000.
22.Pesa kwa ajili ya Kusaidia umaliziaji wa nyumba za walimu Shule
ya Msingi Ntewa A Kata ya Ntuntu,Kijiji cha Ntewa A kiasi cha sh 2,000,000.
23.Pesa kwa ajili ya Kusaidia ujenzi wa madarasa 2 Shule Shikizi
Ititimo Kata ya Issuna,Kijiji cha Issuna A Kiasi cha Sh 2,000,000.
24. Pesa kwa ajili ya Kusaidia ujenzi wa madarasa Shule Shikizi
Mlumbi Katanya Ntuntu,Kijiji cha Ntewa A Kiasi cha Sh 2,000,000.
25.Pesa kwa ajili ya Kusaidia ujenzi wa maabara Shule ya Sekondari
Mang’onyi Shanta Kata ya Mang’onyi,Kijiji cha Tupendane Kiasi cha Sh 4,000,000.
Kwa niaba ya Wananchi wa Jimbo la Singida
Mashariki, Tunamshukuru sana Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.
Mama yetu mpendwa Dkt. Samia Suluhu Hassan na wasaidizi wake wote Serikalini
kwa kuendelea kuboresha maisha yetu Wana Singida Mashariki kwa kuendelea
kutuletea miradi mikubwa ya maendeleo na kushughulikia changamoto za wananchi
katika wilaya yetu. Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020- 2025 inaendelea kutekelezwa.
ISOME NA HII - Majaliwa akerwa uzembe mamlaka za maji
Ndugu wananchi wenzangu wa Singida
Mashariki tunayo kila sababu ya kutoa shukuran kwa Mhe. Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mama yetu mpendwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea
kutupa fedha nyingi kwa ajili ya kutatua miradi ya Maendeleo. Tumuombee Mhe.
Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan Mwenyezi Mungu ampe Afya Njema na kumlinda
vyema ili aendelee na maono yake mazuri katika Kujenga Taifa Letu.
Mhe. Rais wetu Mpendwa Mama yetu Dkt. Samia
Suluhu Hassan ameendelea kusikia kilio chetu kupitia sauti yenu Bungeni.
Ndugu wananchi wenzangu kwa dhati kabisa
nawahakikishia kuwa nitaendelea kuwa sauti yenu Bungeni na kuwawakilisha
ipasavyo kwa Unyenyekevu,Utiifu,Uadilifu na Uaminifu mkubwa.
MUHIMU: Natoa wito kwa watumishi wote na
viongozi ngazi za Vijiji na Kata kuhakikisha kuwa miradi hii iliyoletewa fedha
inasimamiwa vizuri na kwa ufanisi mkubwa ili wananchi wapate huduma hizi kwa
wakati.
0 Comments