TAMISEMI YAWAWEKA KIKAONGONI WASIMAMAZI WA MIRADI YA ELIMU

 

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) imesema haitowavumilia na kufumbia macho viongozi walioshindwa kusimamia na kukamilisha ujenzi wa miundombinu ya shule za awali, msingi na sekondari licha ya maelekezo ya Serikali ya kumaliza ujenzi Disemba 30, 2023.


Rai hiyo imetolewa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za mitaa (TAMISEMI) Adolf Ndunguru wakati akifungua kikao kazi kwa Makatibu Tawala Wasaidizi Elimu na Maafisa Elimu wa Halmashauri zote nchini, na kuwataka kukamilisha miradi hiyo ifikapo Januari 15, 2024

Amesema Serikali imeendelea na utekelezaji wa maboreso ya sekta ya elimu ambapo Shilingi Tilioni 1.41zimekwishatengwa katika kipindi cha mwaka 2020/21 hadi 2023/24 kwajili ya ujezi wa miundombinu ya shule za awali, msingi na sekondari ikiwa ni moja ya hatua madhubuti zinazoendelea kutekelezwa.

Ameeleza kuwa baadhi ya Mikoa ujenzi wa miradi ya Shule upo chini ya 50% licha ya serikali kuelekeza miradi hiyo kukamilika kwa wakati uliopangwa, uzembe ambao kwa wale wanaosimamia miradi hiyo wanapaswa kujitafakari na kuachana na visingizio vya kutokamilisha kazi waliyokabidhiwa kuitekeleza.

“Nasikitika kusema pamoja na dhamira njema ya serikali kutekeleza miradi hiyo, bado miongoni mwenu wachache, kuna viongozi kabisa kusimamia utekelezaji wa miradi hiyo kwa muda ulioapangwa, licha ya maelekezo ya seraikali kumalisha ifikapo Disemba 30, 2023” Amesema Ndunguru

Aidha Ndunguru amewataka viongozi hao kuhakikisha wanasimamia kikamilifu ufundishaji na ujifunzaji, ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua za kinidhamu walimu wasiotekeleza wajibu wao, kuhakikisha wanafunzi wa darasa la kwanza na kidato cha kwanza wanamdu stadi za lugha ya Kingereza ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.

Kwa uapnde wake Mwenyekiti wa maafisa elimu Michael Ligala amesema kiini cha kutokukamilika kwa wakati miradi ya ujenzi wa miuondombinu ya shule ni usimamizi mbovu kwa baadhi yao, huku akiwasihi kwa watakao kumbana na vikwazo vya kutokamilisha miradi hiiyo muda mwingine ulioongezwa kutoa taarifa mapema iwezekananvyo.



TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments