Mkurugenzi mkuu wa IMF
Kristalina Georgieva anasema “katika hali nyingi, AI itazidisha ukosefu wa
usawa kwa ujumla”.
Bi Georgieva anaongeza
kuwa watunga sera wanapaswa kushughulikia “mwenendo unaosumbua” ili “kuzuia
teknolojia dhidi ya kuchochea zaidi mivutano ya kijamii”.
Kuenea kwa AI kumeweka
faida na hatari zake chini ya uangalizi.
IMF ilisema AI
itaathiri idadi kubwa ya ajira – ikiwa ni karibu 60% – katika uchumi wa
juu.Katika nusu ya matukio haya, wafanyakazi wanaweza kutarajia kufaidika
kutokana na ushirikiano wa AI, ambayo itaongeza tija yao.
Katika hali nyingine,
AI itakuwa na uwezo wa kufanya kazi muhimu ambazo kwa sasa zinatekelezwa na
wanadamu.Hii inaweza kupunguza mahitaji ya wafanyikazi, kuathiri mishahara na
hata kumaliza kazi.
Wakati huo huo, IMF
inakadiria kuwa teknolojia hiyo itaathiri asilimia 26 tu ya nafasi za kazi katika
nchi zenye kipato cha chini.
Bi Georgieva alisema
“nyingi za nchi hizi hazina miundombinu au nguvu kazi yenye ujuzi kutumia
manufaa ya AI, na hivyo kuongeza hatari kwamba baada ya muda teknolojia inaweza
kuzidisha ukosefu wa usawa kati ya mataifa”.
0 Comments