TFF yamsimamisha kazi Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Adel Amrouche

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limemsimamisha kazi, Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Mualgeria Adel Amrouche na kumteua, Hemed Suleiman (Morocco) kuwa, Kaimu Kocha Mkuu.

Hayo yanajiri baada ya Shirikisho la Soka barani Afrika kumfungia mechi nane Amrouche kwa kutoa kauli zisizo za kiungwana dhidi ya Morocco.

Ni kuelekea mchezo wa kwanza wa Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika huko nchini Ivory Coast.

Amrouche ameituhumu Morocco kuwa inajipangia muda wa kucheza mechi zake na marefa wa kuchezesha pia akilenga kuaminisha ni kwa sababu hiyo wanafanya vizuri.

Simba wa Atlasi, Morocco wailifunga Tanzania, Taifa Stars 3-0 kwenye mchezo huo wa ufunguzi wa Kundi F Jumatano Uwanja wa Laurent Pokou jijini San-Pedro nchini Ivory Coast.

Mabao ya Simba wa Atlasi yalifungwa na beki wa Al-Shabab ya Saudí Arabia, Romain Ghanem Paul Saïss dakika ya 30, kiungo wa Marseille ya Ufaransa, Azzedine Ounahi na mshambuliaji wa Sevilla ya Hispania, Youssef En-Nesyri dakika ya 80.

Taifa Stars ilimaliza pungufu baada ya kiungo wa Shakhtar Donetsk ya Ukraine, Novatus Dismas Miroshi kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 70 kufuatia kuoneshwa kadi ya pili ya njano.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments