TGNP yaendesha mafunzo uongozi wa kijinsia

MTANDAO wa Jinsia Tanzania (TGNP) unaendesha programu ya mafunzo ya siku kumi kuhusu masuala ya uongozi wa kijinsia, lengo likiwa ni kuwawezesha wanajamii kuthamini nguvu za pamoja na kushirikisha wanawake katika nafasi za maamuzi kama sehemu ya mabadiliko katika jamii na kuwainua kiuchumi.

 Washiriki kutoka nchi mbalimbali za Afrika, ikiwemo Kenya, Uganda, Zimbabwe, Rwanda, Ghana, Burundi, Afrika Kusini, na Nigeria, wamejumuishwa katika mafunzo haya ya uongozi wa kijinsia, yakilenga kukuza mazingira ya kujifunza yenye ufanisi na ushirikiano.

Anna Sangai, Ofisa wa Programu ya Mafunzo wa TGNP, ameeleza kuwa washiriki wamejifunza jinsi jamii inavyoweza kuenzi nguvu za pamoja na kushirikisha wanawake katika nafasi za maamuzi.

Aidha, washiriki walitembelea Kituo cha Taarifa na Maarifa huko Kipunguni kwa lengo la kuelewa jinsi wanawake wanavyojiwezesha kuleta mabadiliko katika jamii, hususan katika kukabiliana na ukatili wa kijinsia, mimba za utotoni, unyanyasaji wa kimwili, na uhifadhi wa mazingira kwa ajili ya kuwawezesha kiuchumi wanawake.

Sangai alisisitiza kuwa wanawake walifundishwa jinsi ya kutengeneza mkaa mbadala kwa matumizi yao binafsi na biashara, hivyo kuchangia katika ukuaji wao kiuchumi. Pia walijifunza kutumia mbolea kuzalisha wadudu kutokana na taka, kuwa chakula cha kuku na kuchangia katika njia endelevu ya upatikanaji wa chakula.

 katika hayo majumuiko ya kujifunza wametumia kama fursa ya kupata taarifa ya ukeketaji, watoto kuozeshwa kwenye umri mdogo, wanaotembea na wanafunzi, vipigo ili kuhakikisha sheria inachukua mkondo wake kwa baadhi ya ambao wamekuwa wakifanya vitendo vya ukatili wa kijinsia” amesema Anna Sangai

 Amesisitiza kuwa Kituo cha Taarifa na Maarifa kinaendeshwa kikamilifu na wanawake, huku Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Katibu wote wakiwa wanawake, hivyo kuonyesha uwezo wa wanawake kuongoza kwa ufanisi na kuleta mabadiliko chanya katika jamii.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments