ARUSHA: Kituo cha Uwekezaji Tanzania(TIC) kimewataka wawekezaji wazawa pamoja na wageni kuchangamkia fursa za uwekezaji zitakazowezesha vijana kupata ajira.
Hayo yamesemwa na Meneja Uhamasishaji na Uwekezaji wa Ndani TIC, Felix John wakati wa ziara iliyofanywa na TIC kwenye kampuni ya ya Hanspaul inayotengeneza magari ya utalii kwa ajili ya mwendelezo wa kampeni ya uwekezaji wa ndani inayofanywa mikoa mbalimbali nchini
Amesema kampeni hiyo ina lengo la kutoa elimu kwa Watanzania kuhusu dhana ya uwekezaji pamoja na kuhamasisha wazawa kushiriki kikamilifu katika uwekezaji wa miradi mbalimbali ya kiuchumi na kuchangia fursa fursa zilizopo.
“Tuna taasisi 12 zimeungana kwa pamoja kufungua fursa za uwekezaji kwa wazawa na wageni, Tanzania ina fursa za uwekezaji karibuni muwekeze,” amesema.
Naye Mkurugenzi wa Hanspaul, Satbir Sighn Hanspaul ameipongeza serikali kwa kuweka mazingira rafiki ya uwekezaji kwa wazawa na wageni, pia amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutaingaza vyema nchi kupitia filamu ya Royal Tour, ambayo imewezesha fursa mbalimbali kufunguka na kuwapa ajira vijana
0 Comments