TPA YASHIRIKI MAADHIMISHO YA WIKI YA SHERIA TANZANIA

 
Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) inashiriki katika Maadhimisho ya wiki ya Sheria Tanzania 2024 inayofanyika Mkoani Dodoma.

Maadhimisho ya mwaka huu yenye kauli mbiu ya “Umuhimu wa dhana ya Haki kwa Ustawi wa Taifa, nafasi ya Mahakama na Wadau katika kuboresha mfumo jumuishi wa haki jinai” yanafanyika sambamba na maonesho ya Wadau katika Viwanja vya Nyerere Square.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa TPA Bw. Nicodemus Mushi amesema, TPA inathamini sana Mchango wa Sekta ya Sheria katika kutekeleza majukumu yake ya kuhudumia Meli na Shehena sambamba na kuendeleza Miundombinu ya Bandari kote Nchini.

“Tunafanya biashara na Wadau wa Kitaifa na Kimataifa ambapo tunaingia Mikataba na makubaliano mbalimbali, hata katika miradi ya kuboresha Bandari zetu tunazingatia Sheria ili pande zote husika ziweze kutimiza Wajibu wake”. Amesema Bw. Mushi.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments