#VIDEO: Msiache Kutumia Ofisi zetu kwa Msaada wa Kisheria

Waziri wa Katiba na Sheria PINDI CHANA amewataka wananchi kuzitumia Ofisi za Msaada wa Kisheria na Madawati ya Jinsia zilizopo katika maeneo yao ili waweze kupata haki zao.

Waziri PINDI CHANA alisema hayo wakati akizindua Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia mkoani Singida.

Mkoa wa Singida ni mkoa wa sita tangu kampeni hii izinduliwe kitaifa, ikiwa na lengo la kutoa maasada wa kisheria kwa wananchi wa mkoa wa Singida walioko pembezoni ambao hawafikiwi na Msaada wa kisheria na ambao hawana uwezo wa kuwalipa mawakili ili waweze kupata haki zao.

Alisema wananchi wengi wanakosa haki zao za msingi kutokana na kukosa maasada wa kisheria au kuwa na uelewa mdogo kuhusu Sheria mbalimbali.

Aidha amesema Mpangoa wa Wizara yake ni kuhakikisha wananchi wanafikiwa na Msaada wa Kisheria na Haki za Binadamu ili kuondoa changamoto zinazowakabili wananchi.

Hata hivyo alisema Wizara pia itaendelea kuweka mikakati na miongozo ambayo itawasaidia wananchi kupata haki zao kwa wakati.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Singida PETER SERUKAMBA alisema kupitia kampeni hiyo Wananchi wengi wa mkoa wa Singida watapata haki zao.

SERUKAMBA alisema wao kama mkoa wataendelea kusimamia Sheria na Haki za Binadamu ili kuondoa changamoto zinazowakabili zinazowakabili wananchi kwa kukosa Msaada wa Kisheria.

Akitoa salamu za Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Singida, Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Mkoa wa Singida ELPHAS LWANJI aliwatoa hofu wananchi kuwa Msaada wa Kisheria ni bure hivyo wananchi wenye changamoto za kisheria wajitokeza kwenye ofisi za Msaada wa Kisheria.

Hata hivyo LWANJI ameishukuru serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuweka mazingira mazuri ya upatikanaji wa Haki katika Jamii.

VIDEO: MSIACHE KUTUMIA OFISI ZETU KWA MSAADA WA KISHERIA

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments