Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana,Ajira na wenye Ulemavu imetoa Takribani Shiling Bilioni 981 kwaajili ya kuwawezesha Vijana katika project mbalimbali zilizopo ndani ya Program ya Building a Better Tomorrow (BBT).
Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu Mh Prof.Joyce Ndalichako katika Warsha ya mapokezi ya Vijana BBT katika shamba la Chinangali II lililopo Jijini Dodoma lililokwenda sambamba na ugawaji wa vifaa vya shamba na kukabidhi barua za umiliki kwa Vijana hao 268.
Na kuongeza kuwa pale kunapokuwa na uhitaji wa Fedha Serikali katika kusaidia malengo ya Vijana wamekuwa wakifanya hivyo.
"Pale ambapo kuna fedha za Serikali ambazo zimekuwa zinaweza kutumika kwa malengo husika tumekuwa tukifanya hivyo, kwahiyo hata Yale mafunzo ya Vijana 74 waliokiwa Kambi ya Bihawana Wizara yangu iliwalipia fedha za kujikimu lakini pia kuna hii project ya kunenepesha mifugo kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi ambapo pia tumewezesha kutoa mafunzo kwa Vijana kwa kunenepesha mifugo ambapo tumetumia Takribani Shiling Bilioni 453. Lakini pia tumewezesha Vijana 234 katika mafunzo ya Mifugo ambapo tumetumia Takribani Shiling Bilioni 234 kwahiyo kwa ujumla Ofisi ya Waziri Mkuu imetoa shilingi Bilioni 981 kwaajili ya kuwawezesha Vijana wetu".
Sambamba na maelezo hayo pia Waziri Ndalichako ametumia nafasi hii kuwasihi Vijana hawa BBT kwenda kufanya Kazi vizuri,kwa bidii na pia kufuata Yale waliyofundishwa.
"Kwahiyo Sasa niwasihi Sana Vijana mwende mkafanye Kazi yenu vizuri,nyie ndio mtakuwa wa kuendeleza Yale mashamba yaliyokuwepo mwanzo au ya kusema Sasa hii program iendelee kwa spidi ya 5G, kwasababu ya mafanikio ambayo mtayaonesha,naomba Sana mjitume katika Kazi zenu,mkafanye Kazi kwa bidii,lakini kubwa zaidi mkafanye Yale mliyofunzwa".
Awali akimkaribisha Mgeni Rasmi, Mh Hussein Bashe ambaye ndie Waziri wa Kilimo amesema kuwa Program hii ya BBT Ina malengo matatu ikiwemo kutengeneza Ajira,Kupunguza Umaskini na Kuongeza Tija.
"Tunapozungumzia BBT sio project yani sio mradi Bali ni program na hii Ina malengo matatu na la kwanza ni kutengeneza Ajira,lengo la pili kupunguza Umaskini na la tatu kuongeza Tija".
Aidha Waziri Bashe ameongeza kuwa walipoanza kuijadili program hii ya BBT walianza kwa kufanya Tafiti kujua kwanini Vijana wengi hawajihusishi na kilimo na waligundua kuwa wengi Wana changamoto ya mitaji, Ardhi na Ujuzi.
"Badala ya kuwa viongozi wanaolaumu kuwa Vijana hawataki kilimo tulifanya Tafiti Vijana hawalimi,tukagundua Mambo matano, la kwanza hawana Ardhi,kijana lazima awe na Ardhi ya kulima,lakini pili lazima awe na Teknolojia itakayomfanya aweze kulima,la tatu huyu kijana lazima awe na mfumo mzuri wa fedha, Sasa tukaona hayo yote tutayatatuaje ndipo tukaanzisha hii program ya BBT".
Akitoa salama za Mkoa, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mh Rosemary Senyamule amesema kuwa mpaka Sasa Mkoa wa Dodoma zimekuja zaidi ya shilingi Bilioni 97 za miradi mbalimbali ya umwagiliaji ikiwemo Chinangali, Membe na Ndogowe.
"Tulikuwa tunahesabu hivi karibuni tuna zaidi ya shilingi Bilioni 97 zimekuja Dodoma kwaajili ya miradi mbalimbali ya umwagiliaji ikiwemo wa Chinangali, Membe,Msagali -Mpwapwa,Kongogo - Bahi na Ndogowe,hii miradi imetufanya kuondoa kabisa mawazo ya njaa kwa Mkoa wa Dodoma hata kuondoa matatizo ya kiuchumi".
Naye Bwana Deo Mwanyika Mbunge na ni Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge Wizara ya Kilimo,Biashara,Viwanda,Mifugo na Uvuvi amesewasihi Vijana hawa kutowaangusha na kutomuangusha Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dkt Samia Suluhu Hassan kwa hii ni Mali ya Watanzania na wao kupata fedha hizi kwaajili mradi kuna wengine wanaweza kuwa wamekosa au kupunguziwa.
"Hivyo Mimi niombe msituangushe,msiwaangushe Watanzania na pia msimuangushe Raisi wetu,hii ni Mali ya Watanzania ninyi mmepewa dhamana msituangushe,ninyi mmepewa fedha hizi kuna wengine wanaweza kuwa wamekosa au kupunguziwa hivyo mkalete matokeo mazuri".
Jumla ya Vijana wote ambao wataanza Kazi ya Kilimo kwa awamu hii 685 lakini wakaokuwa katika shamba la pamoja la Chinangali II ni Vijana 268 ambapo wengine watakuwa katika mashamba yaliyopo Kijiji cha Ndogowe.
0 Comments