Kufuatia Mvua
zinaendelea kunyesha mkoani Morogoro Mkuu wa wilaya ya Mvomero ameiagiza
halmashauri ya wilaya hiyo kuhakikisha inagawa haraka viwanja kwa waathirika wa
mafuriko yaliyotokea wilayani humo kata ya Mvomero ambapo zaidi ya watu 500
wanaokadiriwa kukoswa maakazi kwa sababu ya mafuriko.
DC Nguli ametoa
maagizo hayo wakati alipotembelea baadhi ya maeneo yaliyoathiriwa na mvua
ambazo zimeleta athari kubwa ikiwemo nyumba zao kubomoka jambo lililosababisha
Wananchi hao kukosa makazi pamoja na huduma za kijamii.
Kwa upande wake
mwakilishi wa bodi yamaji ya bonde la Wami Ruvu Antony Lugai amesema chanzo cha
maji haya ni baadhi ya mito kujaa michanga hivyo kushindwa kupeleka maji kwenye
mkondo unaotakiwa jambo lililosababisha maji kuelekea katika makazi ya watu.
#VIDEO: Wananchi Mkoani Singida Wametakiwa Kuendelea Kutoa Taarifa Kwa Jeshi La Polisi
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI
Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516
0 Comments