Wachezaji 10 wakuchungwa Afcon

MAKALA: KOMBE la Mataifa ya Afrika la CAF 2023 linalofanyika 2024,linatarajiwa kuchukuwa sura mpya kutokana na kukithiri kwa nyota wengi wanaocheza soka nje ya Afrika wanaotarajiwa kukiwasha katika michuano hiyo.

Senegal ndio mabingwa watetezi, na kikosi chao kilichojaa nyota wengi kinawafanya kuwa miongoni mwa wanaopewa nafasi kubwa kuelekea michuano hiyo. Simba wa Teranga hawako peke yao katika kujivunia vipaji vya hali ya juu duniani, wakifanikisha AFCON ambayo kwa mara nyingine ni ngumu kutabiri.

Kutoka Ligi Kuu England, Serie A na kwengineko hawa ni wachezaji 10 wanaotarajiwa kuangazia michuano hiyo na pengine hata kunyanyua kombe katika michuano hiyo itakayoanza Januari 13 na kutamatika Februari 11 Côte d’Ivoire.

VICTOR OSIMHEN (NAPOLI)

Nyota huyo anayekipiga Napoli ya Italia, ndiye anayeshikilia tuzo ya mchezaji bora Afrika kwa sasa. OSIMHEN ,24, alikuwa sehemu muhimu msimu uliopita Napoli ilipochukuwa ubingwa wa Serie A akiwa na mabao 26.

Osimhen ambaye bado amevaa kinyago cha kujikinga usoni licha ya kupona jeraha la tundu la jicho lililomfanya kuwa nje ya AFCON 2021 ametia saini kandarasi mpya wiki iliyopita. Tayari ana mabao 20 katika mechi 27 alizoichezea Nigeria na anaonekana kuwa mchezaji wa ajabu kwa kuvuka rekodi ya Rashidi Yekini ya kufunga mabao 37 akiwa na Super Eagles.

MOHAMED SALAH (LIVERPOOL)

Misri haijatwaa taji hilo tangu 2010, hata hivyo walipoteza mara ya mwisho 2021 dhidi ya Senegal kwa mikwaju ya penalty 4-2. Mohamed Salah alikuwa sehemu ya kikosi hicho, na kile kilichokosa ubingwa huo mwaka 2017 dhidi ya Cameroon kwa kufungwa mabao 2-1.

Salah atakuwa na shauku ya kuhakikisha Misri hairudii makosa hayo kwa kuukosa ubingwa huo mara ya tatu nay eye akiwepo. Kiwango chake cha sasa kwa Liverpool kinaonesha kuwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 ana nia kuliheshimisha taifa lake.

SADIO MANE (AL-NASSR)

Mane alitangazwa kuwa mchezaji bora wa Afrika mara mbili. Mwaka 2019 na 2022 mara baada ya kubeba ubingwa wa Afrika kwa kuifunga Misri. Mane alifunga penalty ya ushindi na kuiongoza Senegal kunyakua taji lao la kwanza la AFCON.

Baada ya muda mfupi akiwa Bayern Munich, fowadi huyo alijiunga na Cristiano Ronaldo katika klabu ya Al-Nassr ya Saudia na tayari ameshazifumania nyavu mara 12. Akiwa na mabao matatu katika mechi za hivi karibuni Senegal, Mane anaonekana kuwa na kiwango bora cha kutetea ubingwa wa nchi yake.

RIYAD MAHREZ (AL-AHLI)

Kama ilivyokuwa kwa Sadio Mane, Riyad Mahrez alielekea Saudi Pro League msimu wa joto. Wawili hao pia wameonja utukufu wa AFCON huku Mahrez akiwa nahodha wa Algeria hadi mafanikio yao ya 2019.

Winga huyo alifunga mara moja katika kampeni zao hatua ya makundi, kisha tena katika hatua ya 16, kabla ya mkwaju wake wa faulo katika dakika za lala salama kuhitimisha ushindi dhidi ya Nigeria katika nusu fainali.

Katika fainali, bao la dakika ya pili la Baghdad Bounedjah lilitosha kushinda Senegal na kupata taji la kwanza la AFCON tangu 1990.

ACHRAF HAMIKI (PSG)

Beki wa kulia wa PSG Achraf Hakimi alikuwa muhimu kwa Morocco kuwa taifa la kwanza la Afrika kutinga nusu fainali ya Kombe la Dunia nchini Qatar mwaka 2022. Ilikuwa kazi kubwa na Hakimi alikuwa na wakati mzuri alipofunga Panenka katika ushindi wa hatua ya 16 dhidi ya mabingwa wa 2010 Uhispania.

Sasa jukumu lao litakuwa kutafsiri mafanikio hayo kwenye Afcon huku Morocco ikitwaa ubingwa wa AFCON mwaka wa 1976. Lakini kwa Hakimi nyota wa kikosi ambacho pia kinajivunia kuwa na wachezaji bora, inaweza kuwa mashindano ya kukumbukwa kwa Simba ya Atlas.

INAK WILLIAM (ATHLETIC CLUB)

Huyu ni mmoja wa wachezaji wenye ubora ndani ya La Liga atapamba AFCON kwa mara ya kwanza mwezi huu, akiwa Ghana kwa mara ya kwanza mnamo Julai 2022 kufuatia ahadi aliyomuahidi babu yake ya kucheza michuano hiyo.

Fowadi huyo wa Athletic Bilbao, ambaye alichezea Uhispania U-21, tangu wakati huo amecheza mechi 12 kwa nchi yake ikiwa ni pamoja na Kombe la Dunia la FIFA nchini Qatar.

Williams, kaka wa nyota mwenzake wa Athletic Bilbao na Uhispania, Nico, alifunga bao lake la kwanza la kimataifa katika ushindi wa 1-0 wa kufuzu kwa Kombe la Dunia dhidi ya Madagascar na aliweka wakfu kwa babu yake aliyeaga dunia mapema mwaka wa 2023.

FRANK ANGUISSA (NAPOLI)

Mchezaji pekee wa Cameroon katika timu bora ya 2023 ya CAF, Frank Anguissa ndiye hirizi ya taifa lake.

Katika ngazi ya klabu, pamoja na Osimhen, aliisaidia Napoli kushinda taji lao la kwanza la Serie A tangu Diego Maradona alipowaongoza Scudettos mnamo 1987 na 1990.

Kama mtekelezaji wa safu ya kati ambaye anafanya kazi chafu na mara chache haangazii vichwa vya habari, Anguissa ni mojawapo ya majina ya kwanza kwenye anga za Napoli na Cameroon.

SERHOU GUIRASSY (VFB STUTTGART)

Wakati wa mapumziko ya msimu wa baridi, Guirassy anashika nafasi ya pili kwenye orodha ya wafungaji wa Bundesliga akiwa na mabao 17 dhidi ya 21 ya Kane.

Mchezaji huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Ufaransa atakumbukwa sana na Stuttgart atakapocheza mechi yake ya kwanza ya AFCON baada ya kuichezea Guinea kwa mara ya kwanza 2022.

PATSON DAKA (LEICESTER CITY)

kwa zambia, daka amefunga mara tano katika michezo yake mitatu iliyopita na anabeba matumaini ya taifa ambalo lilishinda taji la Afcon mnamo 2012.

YOUSSEF MSAKNI (AL-ARABI)

Nguvu ya Tunisia iko katika ubora wao uwanjani, lakini nahodha Youssef Msakni bila shaka ndiye mchezaji bora katika timu ambayo mara kadhaa imekuwa ikifika hatua ya mtoano AFCON. Mabingwa kwa mara ya kwanza mwaka wa 2004, Eagles of Carthage wamefika hatua ya robo fainali mara saba.

Mara moja tu ndio wamesonga mbele zaidi mnamo 2019 walipomaliza nafasi ya nne, lakini mechi mbili mfululizo za Kombe la Dunia zinawafanya kuwa moja ya timu bora barani Afrika. Hadi nafasi ya 29 katika viwango vya FIFA, ikishika nafasi ya nne kati ya mataifa ya Afrika, Tunisia inatarajiwa kutoka katika Kundi E ambapo itamenyana na Mali, Afrika Kusini na Namibia.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments