Wadau wa Demokrasia wakoshwa na Samia

WADAU wa Demokrasia ndani na nje ya nchi wamesifu Rais Samia Suluhu Hassan kusimamia sera ya R nne.

Pia, wamepongeza kuruhusu uhuru wa Habari na kujieleza, kuruhusu mikutano kwa vyama vya siasa na kutoa nafasi zaidi kwa wanawake katika ngazi za uongozi.

Wakizungumza katika mkutano maalum wa Wadau wa Demokrasia kujadili miswada ya sheria za vyama vya siasa iliyowasilishwa Novemba 10, mwaka 2023, Profesa Alexander Makulilo mbobezi wa Sayansi za Siasa kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam amesema utawala wa Rais Samia umebadilisha upepo wa siasa kwa kuruhusu mikutano ambayo awali ilizuiliwa na mtangulizi wake.

“Sera ya R 4 za Rais inayohusu upatishi, kuvumiliana, kuishi pamoja na kujenga nchi, hotuba ya Rais Samia aliyotoa Machi 19, 2021 alisema ni wakati wa kuzika tofauti na kuwa wamoja, kufarijiana, kutunza utu wetu, utanzania wetu….. ” amesema Makulilo

Nae Mbunge wa Malawi Suzan Dossi amesema Rais Samia amekua chachu ya wanawake kuonyesha kuwa wanaweza wakishika nafasi za uongozi si tu kwa Tanzania hata nchi nyingine barani Afrika.

Amesema Rais Samia amekua mfano kuigwa kwa kuongeza wigo wa wanawake katika Baraza la Mawaziri akimtolea mfano Waziri wa Ulinzi Stergomena Tax ambae amepewa kusimamia kitengo hicho nyeti.

Aidha amesema ukatili wa kiuchumi unanyima wanawake fursa za kushinda katika chaguzi za awali ndani ya chama.

Amesema, Malawi hakuna viti maalum, ndio wanapambana kuhakikisha uchaguzi wa 2025 nchini Malawi kuweka na viti hivyo.

Hata hivyo, amesema viti maalum ni vizuri kwa kuwa vinaongeza wigo wa wanawake bungeni lakini ni vyema wanawake wakawezeshwa kwenda kuwania ubunge kwenye majimbo.

“Wanawake wengi wanaogopa kuingia kwenye siasa kutokana na kuogopa kupewa majina mabaya na kudhalilishwa,” amesema Suzan.

Kwa upande wa Mbunge wa Kenya, Catherine Mumma amesema Rais Samia ameonyesha njia kwa kuwapa wapinzani uhuru wa kuongea.

” Tanzania ni jirani mzuri, Rais Samia ni kiongozi mzuri, tunasherehekea juhudi zake anazoonyesha katika uongozi;…..” amesema Catherine.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments