Wanafunzi 32,000 waanza masomo Arusha

WANAFUNZI  32,000 wa darasa la kwanza wameanza masomo katika Halmashauri ya Jiji la Arusha katika mwaka wa masomo 2024/25 idadi ambayo ni kubwa na imevunja rekodi kwani haijawahi kutoa kwa kipindi kirefu.

Akizungumza na HabariLeo, Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Juma Hamsini amesema kuwa shule zote katika jiji hilo zimefunguliwa kwa muhula mpya wa masomo kwa waafunzi wanaojinga na shule za awali ,msingi na sekondari.

Hamsini alisema kwa upande wa Jiji la Arusha pekee wao wameweza kuandikisha zaidi ya wanafunzi 32,000 wanaotarajiwa kujiunga na masomo yao katika mwaka wa masomo 2024 ambapo ni kiwango kikubwa kuwahi kufikiwa.

” Hadi Januari 5 mwaka huu wanafunzi wanao jiunga na masomo ya kidato cha kwanza katika shule zetu za sekondari zilizo ndani ya Jiji la Arusha ni wanafunzi 14,471 ,Wanafunzi walioandikishwa kujiunga na shule za msingi darasa la kwanza ni wanafunzi 11,521 na wanafunzi waliyoandikishwa kujiunga na masomo ya awali yani chekechea ni  8,160″. Alisema Hamsini.

Akifafafanua juu ya idadi hiyo ya wanafunzi hao waliyochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza  ambapo kwa idadi yao wote ni 14,471 ambapo wavulana ni 6,948 na wasichana ni 7,523 waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza kwa mwaka 2024 katika shule 31 za sekondari za kutwa katika Halmashauri ya Jiji la Arusha.

Aidha alifafanua kuwa makadilio ya wanafunzi waliyo kuwa wamekusudiwa kuandikishwa kuanza darasa la kwanza kwa mwaka 2024 ni jumla ya wanafunzi 14, 584 lakini hadi sasa wameandikisha wanafunzi 14,121 ambayo ni sawa na asilimia 78.15% ya wanafunzi waliyo andikishwa kuanza darasa la kwanza ambapo wavulana ni 5,815 na wasichana ni 5,606.

Pia ameeleza kuwa katika wanafunzi wa darasa la awali walilenga kuandikisha wanafunzi 15,191 kwa mwaka 2024 la hadi sasa wameandikisha wanafunzi 8,160 ambayo ni sawa na asilia 53.72% ya wanafunzi hao ambapo wavulana ni 4,121 na wasichana ni 4,041.

Aidha Hamsini aliwasihi wazazi ambao bado hawaja wandikisha watoto kujiunga na masomo wafanye haraka na kwa wazazi ambao tayari wamesha wandikisha watoto wafanye mahitaji kwa wakati ili kutowachelewesha watoto katika mashomo kwa maana Jiji la Arusha linejipanga vyema katika utoaji wa elimu bora kwa wanafunzi na kwawakati.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments