WATU wanne wamekamatwa kutokana na kuharibu miundombinu ya reli ya kisasa ya treni ya umeme (SGR), kati ya hao watatu walikamatwa katika eneo la Ngerengere mkoani Morogoro wakiwa na vipande 396 vya nondo na mmoja katika eneo la Makulu mkoani Dodoma kwa kubomoa nguzo nane za uzio wa SGR.
Kamanda wa Kikosi cha Polisi Reli Tanzania, Sebastian Mbuta amejionea uharibifu huo baada ya kufika eneo la tukio pamoja na kufika Kituo cha Polisi Ngerengere kushuhudia nondo hizo zilizokamatwa zenye ukubwa wa milimita 16 ambazo zilijengea uzio kuzuia wanyama waharibifu wasikatize wakiwemo tembo.
Mbuta amethibitisha kutiwa mbaroni kwa watuhumiwa hao ambao ni Florah Mbago (39), mkazi wa Kiburumo Ngerengere na Juma Kijiti (66), mkazi wa Mgudeni Ngerengere ambao waliokutwa na vipande 17 vya nondo za ukubwa wa milimita 16, mali ya Kampuni ya Rubis ya nchini Afrika Kusini waliopewa kandarasi ya kujenga kilometa 16 za uzio huo wa kuzuia wanyamapori kuvuka upande mmoja kwenda mwingine na kuharibu reli.
Amemtaja mtuhumiwa mwingine, Living Emmanuel (20) ambaye ni fundi wa kujenga uzio na mkazi wa Chamwino Ngerengere, ambaye alikamatwa akiwa na vipande vya nondo vilivyokatwa 379 na mkoani Dodoma pia amekamatwa Elia Elias (24) eneo la Makulu akibomoa nguzo nane za uzio wa reli hiyo kwa kuzivunja na nyundo ili kuchukua nondo zilizomo ndani yake kwa ajili ya chuma chakavu.
mesema upelelezi wa mashauri hayo utakamilishwa kwa haraka ili watuhumiwa wafikishwe mahakamani.
0 Comments