Hii ni baada ya Anjella kudai kwamba ndoto
yake ya muda mrefu imekuwa kufanya kolabo na Zuchu lakini pia akafichua kwamba
juzi kati walikutana lakini akaogopa kumwambai suala kama hilo.
“Natamani sana kufanya kolabo na Zuchu, ila
juzi nimekutana naye kwenye studio Fulani lakini sikuweza kumwambia hili suala,
nitafurahi sana hili likija kutokea,” Anjella alisema.
Baadaye hili ungamo lilimfikia Zuchu ambaye
kupitia instastory yake alijibu akionekana kukubali kufanya kolabo hiyo ili
kutimiza ndoto ya muda mrefu ya malkia mwenzake.
Zuchu aimtaka Anjella kutuma wimbo ili
ausikize na kujua ni wapi ataongeza mishororo yake katika harakati nzima ya
kutengeneza ngoma ya kikoa.
“Tuma wimbo dadangu, hebu na tuifanye,” Zuchu
aliandika akimtag Anjella.
Kwa muda mrefu, wengi wamekuwa wakifikiria
kwamba wawili hao hawako katika hali nzuri ya maelewano kutokana na hali ambayo
walijikuta.
Itakumbukwa Anjella alikuwepo kama mmoja wa
wasanii waliokuwa chini ya lebo ya Konde Music Worldwide inayomiliiwa na
Harmonize wakati huo huo Zuchu yuko chini ya WCB Wasafi inayomilikiwa na
Diamond Platnumz.
Kutokana na Diamond na Harmonize kutokuwa
na ushirikiano mwema kwenye tasnia ya muziki, baso moja kwa moja mashabiki
wengi walikuwa wakijua kwamba mtu yeyote ambaye yuko kwenye lebo ya WCB Wasafi
moja kwa moja anakuwa adui kwa yule aliyeko Konde Gang pasi na kujali kiini cha
ugomvi wa wamiliki wa lebo hizo.
Lakini baada ya Anjella kutoka mwaka juzi, inaonekana amepata uhuru kabisa wa kujiamulia kile ambacho anakitaka, na kuweka wazi kwamba anataka kolabo na Zuchu ni moja ya uamuzi wake wa kujizungumzia pasi na vikwazo akiwa kama msanii huru.
0 Comments