50% ya Wanahabari wakumbwa na madhila kazini

DAR ES SALAAM: Nusu ya waandishi wa habari nchini Tanzania wameripoti kutishiwa na  kunyanyaswa wanapokuwa wakitimiza majukumu yao ya kazi

Akizungumza Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi  ya Twaweza Aidan Eyakuze amesema katika utafiti waliofanya jijini Dar es Salaam, asilimia 50 ya waandishi wa habari nchini Tanzania wameripoti kukumbana na vitisho, manyanyaso, mateso au kushambuliwa katika kazi zao.

“Wawili kati ya 10 sawa na asilimia 22  wamekamatwa au kuzuiliwa na mamlaka, na idadi sawa na hiyo wamekumbana na unyanyasaji wa kijinsia  ambao ni saw ana asilimia 20 au kunyang’anywa vifaa vyao vya kazi ni asilimia 20.

Amesema, Twaweza ikishirikiana na MISA-TAN, Jamii Forums, UTPC na TAMWA wametoa matokeo hayo kwenye jarida la utafiti lenye kichwa cha habari Sautiza Waandishi: Uzoefu na maoni ya waandishi wa habari wa Tanzania.

Jarida hilo linawasilisha takwimu kuhusu uzoefu na maoni ya waandishi wa habari wa Tanzania. Maoni yalikusanywa kutoka kwa kwa wanahabari 1,202 wakiwemo waandishi wa habari, wahariri na wanablogu.

“Kati ya Waandishi wa Habari 1,202 waliohojiwa na jarida hilo imebaini baadhi ya Waandishi wa Habari hawana ajira za kudumu ambapo waandishi wawili kati ya 10  ndio wenye ajira zakudumu zenye mkataba wa ajira,”amesema.

Amesema, mahojiano yalifanyika kwa njia ya simu kati ya Septemba 23 na Novemba 7, 2023. Waandishi wengi wa habari wana ajira zisizo za kudumu, na zisizo za uhakika. Wawili kati ya 10 sawa na asilimia 20 wanataja kuwa ajira zao ni za kudumu, ikilinganishwa na sita kati ya 10 sawa na asilimia 60  wanaosema ni za muda na wawili kati ya 10 sawa na asilimia 18 wanaosema wanaitwa kazini pale tu wanapohitajika.

Aidha,  Eyakuze amesema asilimia 50 ya Waandishi wa Habari  wanayo mikataba iliyosainiwa. Waandishi wengi wa habari asilimia 63 wanasema ni vigumu kujipatia kipato kinachokidhi mahitaji muhimu kupitia uandishi wa habari, wakati wachache asilimia tano wanasema si tatizo, huku mmoja kati ya waandishi watatu sawa na asilimia 36 wana kazi nyingine inayowalipa mbali na kazi yao ya uandishi.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments