Andreas Brehme: Mfungaji bao la ushindi Ujerumani afariki dunia

BEKI wa Ujerumani, Andreas Brehme aliyefunga bao la ushindi katika fainali ya Kombe la Dunia mwaka 1990 dhidi ya Argentina amefariki dunia.

Brehme ,63, beki wa kushoto alifunga mkwaju wa penalti dakika ya 85 huku vijana wa Franz Beckenbauer wakiilaza Argentina ya Diego Maradona 1-0 mjini Rome.

Beki huyo aliichezea Ujerumani michezo 86 na pia alishinda Bundesliga akiwa na Kaiserslautern na Bayern Munich, pamoja na taji la Serie A akiwa na Inter Milan kabla ya kustaafu 1998.

Bayern walitoa heshima kwa mchezaji wao wa zamani, wakisema: “FC Bayern wamehuzunishwa sana na kifo cha ghafla cha Andreas Brehme. Tunatuma salamu zetu za rambirambi kwa familia yake na marafiki.

“Andreas Brehme atakuwa daima mioyoni mwetu, kama mshindi wa Kombe la Dunia na, muhimu zaidi, kama mtu wa pekee sana. Atakuwa sehemu ya familia ya FC Bayern milele. Pumzika kwa amani, Andi!”

Alifunga katika nusu fainali ya Kombe la Dunia la 1990 dhidi ya Uingereza, ambayo Ujerumani ilishinda kwa mikwaju ya penalti.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments