CCM MKOA WA SINGIDA YATATUA MGOGORO WA STENDI YA MABASI WILAYANI MANYONI MKOANI SINGIDA.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Singida MARTHA MLATA ameagiza Malori yote yanayopaki kwenye Stendi ya Mabasi wilayani Manyoni kuondolewa ili kuleta usalama kwa abiria na watumiaji wengine wa Stendi hiyo.

MLATA alitoa agizo hilo wakati akiwa katika Ziara yake ya kukagua Miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa serikali kupitia Ilani ya CCM wilayani Manyoni.

Alisema sio jambo jema kwa Mabasi na Malori kupaki katika Stendi hiyo ambayo ilitengwa kwa ajili ya mabasi tu.

MLATA alisema kama ni suala la Halmashauri kuongeza mapato kupitia Ushuru wa Malori hayo, watafute eneo jingine kwa ajili ya Malori ili kuleta usalama kwa watumiaji wa Stendi hiyo ya Mabasi.

Baadhi ya watumiaji wa Stendi hiyo walisema  usalama katika Stendi hiyo umekuwa mdogo kutokana na Mabasi, Malori mizigo na mafuta kupaki kwa pamoja katika Stendi hiyo.

Waliongeza kuwa kutokana na Malori hayo kupaki kwenye Stendi hiyo imesababisha baadhi ya Mabasi kupitiliza bila kuingia ndani ya Stendi na wakati mwingien kushusha abiria nje ya Stendi.

Hata hivyo wameiomba serikali kuwasaidia kutatua changamoto hiyo ya Malori ambayo pia yamekuwa yakiiharibu Stendi hiyo kutokana na uzito wa mizigo yanayobeba.

Kwa upande wake uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni walisema wanaendelea kuweka mikakati ya kuhakikisha wanatenga eneo jingine ambalo Malori hayo yatakuwa yanapaki.

Ziara hiyo ya Kamati ya Siasa Mkoa wa Singida ilitembelea Kituo cha Afya Kata ya Sanza, ambapo baadhi ya wajumbe wa Kamati hiyo waliishukuru serikali kwa kuendelea kutekeleza  Miradi ambayo inawaondolea adhaa wananchi ya kufuata huduma za Afya na kijamii umbali mrefu.

YOHANA MSITA ambaye ni MNEC wa Mkoa wa Singida alisema Miradi hiyo ni lazima itunzwe ili wananchi wapate huduma stahiki za kijamii kwa muda mrefu kwani lengo la serikali ni kuwaondolea changamoto mbalimbali na kusogeza huduma katika maeneo yao
                      
Picha Mbali Mbali za Matukio Katika Ziara Hiyo 




















TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments