DAR ES SALAAM: CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimewataka CHADEMA kuacha kigeugeu, na kudai kuwa hawajui wanachokitaka licha ya mswada wa sheria uliopitishwa bungeni kuwa na faida kubwa kwao na vyama vingine vya upinzani.
Akizungumza na Wana CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Abdulrahaman Kinana amesema CHADEMA wanaandamana kupinga miswada lakini hapo hapo wamepeleka watu wa kutoa maoni ya mswada bungeni.
Kinana amesema, miswada mitatu iliyopelekewa bungeni na ijumaa imepitishwa na wabunge, vyama vingine vya siasa vilieleza wanavyoifahamu miswada hiyo, kwa bahati mbaya wengine CHADEMA wanapotosha, na kwa bahati mbaya zaidia wameandaa utaratibu wa kuandamana kupinga.
“CHADEMA hawaeleweki wanataka nini, hapo hapo wanaandamana, hapo hapo walipeleka watu bungeni kutoa maoni yao, hapo hapo wanataka maboresho ya sheria, hapo hapo wanaandamana kupinga muswada wa sheria, hawaeleweki wanataka nini?” amesema Kinana
Amesema katika mchakato wa maridhiano CHADEMA iligomea kushiriki baadhi ya vikao vya maridhiano hata hivyo CHADEMA bado waliitwa na Rais Samia ikulu akawasikiliza hoja zao.
0 Comments