DC KASSANDA AWASILISHA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM KATIKA KIKAO CHA HALMASHAURI KUU YA CCM WILAYANI MAGU.

Mkuu wa Wilaya ya Magu Rachel Kassanda amesema katika kipindi cha Juali hadi Disemba , 2023 Wilaya ya Magu ilipokea jumla ya Shilingi Bilioni 29.1 (29,106,771,919) kwaajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo katika sekta za utawala , afya , elimu , maji na barabara.

DC Kassanda ameyasema hayo wakati akiwasilisha utekelezaji wa ilani ya Chama cha mapinduzi CCM katika kikao cha Halmashauri kuu ya CCM Wilaya ya Magu kilichofanyika katika umbumbi wa CCM Wilayani humo.

Akiwasilisha utekelezaji wa ilani hiyo DC Kassanda amesema katika kipindi kuanzia julai hadi Disemba , 2023 Halmashauri ya Wilaya ya Magu imepokea ilipokea kiasi cha

shilingi 808,468,097 kwaajili ya ujenzi wa nyumba ya mkurugenzi kiasi cha shilingi 180,000,000. na jengo la ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Mgu katika sekta ya utawala kiasi cha shilingi 628,468,097.

Amesema katika sekta ya afya Halmashauri imeweza kutekeleza miradi yenye jumla ya shilingi Bilioni 2.2 ikiwa ni ujenzi wa miundombinu katika zahanati , ujenzi wa uzio katika kituo cha afya Kisesa na ununuzi wa vifaa katika vituo vya afya vya Kisesa, Kahangara, Shishani, Kabila na Lugeye.

Aidha katika sekta ya elimu DC Kassanda amesema Halmashauri imeweza kutekeleza miradi yenye jumla ya shilingi Bilioni 2.6 ikiwa ni ujenzi wa vyumba 67 vya madarasa ,

ukamilishaji wa vyumba 15 vya madarasa , ukarabati wa vyumba vya madarasa 24 ujenzi wa nyumba 7 za walimu na ujenzi wa matundu 77 ya vyoo katika shule mbalimbali za msingi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Magu Simon Mpandalume amewataka viongozi wa CCM Wilaya ya Magu kutangaza mazuri yanayofanywa na Mwenyekiti CCM na Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh. Dkt Samia Suluhu huku akimshukuru Rais kwa kuendelea kuleta fedha nyingi kwaajili ya miradi ya maendeleo Wilayani Magu.

Amesema viongozi wa CCM wana kazi kubwa ya kwenda kusema yale mazuri yote yanayofanywa na Mh Rais Wilayani Magu na kutangaza miradi yote inayotekelezwa Wilayani hapa " Kama tuna zahanati tukaseme zahanati zimejengwa , madarasa yamejengwa tukaseme tuwaambie wananchi wawe na taarifa hizo" amesema.







TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments