Maharage Kupanda Bei

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amewataka wananchi wa mkoa huo kujiandaa na bei ya juu ya maharage

Akizungumzia suala la sukari katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo Februari 19, 2024 katika uwanja wa Msufini Chamazi jijini Dar es Salaam, Chalamila amesema kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha bei ya maharage pia itapanda.

“Ni kama vile ilivyo mwaka huu wa fedha mwaka huu maharage yatakuwa ghali sana, kwa sababu huko (mashambani) mvua imenyesha kubwa na maharage yameathirika sana, kwa hiyo tujiandae pia kwa bei ya maharage baadaye kwa sababu ya hali ya tabianchi.

Chalamila yupo katika ziara ya mkoa mzima wa Dar es Salaam kukagua kuzindua na kuweka mawe ya msingi ziara ambayo imeanza leo Februari 19, 2024.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments