TABORA: Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tabora na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM, Hassan Wakasuvi amefariki dunia leo mkoani Tabora.
Chama cha Mapinduzi CCM kikiongozwa na Mwenyekiti wake Rais, Samia Suluhu Hassan ametoa pole kwa familia pamoja na ndugu jamaa na marafiki wa marehemu.
Aidha taarifa iliyotolewa na CCM imeeleza kuwa Chama hicho kinamtambua Wakasuvi kama mtu mtii, mzalendo na muaminifu kwa Chama chake na Taifa kwa ujumla.
0 Comments